Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Thursday, July 5, 2012

ENDELEA KUMFAHAMU SANGWINI......


Na Nelson Faustin.
a.k.a Meku Mtanzania.

Wapenzi wasomaji wa OHAYODA, naamini umeanza kufuatilia somo hili kwa ukaribu sana, Leo tumalizie sehemu yetu ya kwanza kwa kuangalia zile Sifa njema za sangwini  hapa………………….
·      
     -Sangwini anaingilika kwa uraisi sana kwa wakati wowote kwani kwa kawaida huwa anatenda kwanza na anawaza baadaye.
·      -  Ni mtu wa tabasamu wakati wowote.
·        -Ni bingwa wa kutengeneza mitandao (networking) kutokana na tabia yake ya kujichanganya na watu wa kada zote.
·       - Ana hali ya udadisi sana hata kwa mambo yasiyomuhusu.
·      -  Ana hisia za hali  ya juu sana.
·        -Ni mrahisi sana kuchangamkia jambo hata kwa yale asiyojua yametokea wapi.
·        -Huyu mwanadamu anayeitwa sangwini ni mwenye moyo wa kutetea kweli hata kwa watu wasio na uhusiano wa karibu naye.
·        -Kwa kawaida haweki fundo moyoni kwani kila kinachomwingia lazima kinatoka kutokana na hali yao ya kuwa na hisia za hali ya juu na kukosa usiri.
·        -Ameumbiwa uwezo wa kuweza kuvaa hisia na uhalisia nyingine. (Ni waigizaji wazuri)
·        -Katika swala la imani, sangwini ana imani ya hali ya juu sana.
·        -Ana nguvu kubwa ya kushawishi wengine kwa kile wanachokiamini.
·        -Katika swala la biashara ana nguvu sana na pia ni mziri sana katika kutia chachu maono, sheria au sera mbalimbali katika jamii.
·        -Amejaliwa vipaji vingi (master talented).
·        -Kwa  nia njema kabisa huwa wanakuwa maarufu na wanapenda hali hii.
·        -Ana ujasiri sana hasa mbele za watu.
·        -Walivyo ni sawa na kusema, niangalieni mimi….
Ndugu msomaji, katika kipindi kijacho tutajifunza sasa madhaifu ya sangwini kwani hakuna mwanadamu aliyekamilika……………Tuonane kipindi kijacho.
Kumbuka: Ulivyo ni kwa sura na mfano wa Mungu usidhirahau bali uwe bora kutokana na ubora Mungu aliokuumbia.
                                                                                        Na Neno Litaendelea..................................

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda