Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Friday, July 13, 2012

DONDOO ZA SHERIA: UNAPOKAMATWA NA POLISI


 Raia ana haki ya kumwomba askari ajitambulishe kwako. Mwulize jina lake Mwulize namba yake ya uaskari Raia ana haki ya kujulishwa kwanini anatiliwa mashaka ama kukamatwa.
Raia ana haki ya kuwajulisha ndugu, jamaa ama sehemu anakofanyia kazi kwamba ama amekamatw na polisi ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa.
Raia ana haki ya kuomba na kupewa dhamana wakati akiwa kituo cha polisi ama Taasisi ya kuzuia rushwa. Hutakiwi kutoa fedha kama dhamana uwapo kituo cha polisi ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa, isipokuwa maelezo utakayoandika.
Raia ana haki ya kuwaelezwa  na polisi ama Maafisa wa Kuzuia Rushwa kwamba lolote atakalosema
linaweza kutumiwa kama ushahidi mahakamani, na asiburuzwe kuandika tu. Raia ana haki ya kuomba Wakili wake awepo kituo cha polisi ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa wakati anatoa maelezo yake.
Raia ana haki ya kuyasoma kabla ya kutia sahihi yake. Raia ana haki ya kudai risiti ya orodha ya vitu vyake/fedha zake alizozitoa ama kukabidhi kituo cha polisi ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa.
Raia kama ni mwanamke ana haki ya kupekuliwa na polisi wa kike, na iwapo hakuna polisi mwanamke, basi mwanamke yeyote na vile vile kwa mwanamume.
Raia ana haki ya kufikishwa mahakamani katika muda usiozidi saa 24 tangu alipokamatwa n kufikishwa kituo cha polisi.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda