Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Friday, July 27, 2012

AFYA KWANZA:AINA YA KWANZA YA KISUKARI.


 

Na Bearice Githiri-HLH
Ugonjwa wa kisukari umekuwa janga kubwa duniani kote. Zaidi ya watu milion 366 tayari wanaugua na zaidi wataendelea kuugua ikiwa dunia haibadilisha mienendo ya maisha. 

Kama mtakumbuka makala ya kwanza katika AFYA KWANZA tulizungumzia ugonjwa wa kisukari. Leo nazungumzia wagonjwa wakisukari haswa Type 1 au (aina ya kwanza). Hii aina ya kisukari hupata watu kuanzia umri wakuzaliwa hadi miaka 35, pia lazima hawa watu watumie insulin ambayo ipo katika dawa ya maji na huchomwa mwilini kila siku. 
Type 1 ya kisukari inaweza kutokana na;
  1.   Asilimia kubwa haijulikani sababu.
  2.   Lishe mbaya pindi mama anapokuwa mjamzito.
  3.   Viral infections.
  4.   Kumwanzishia mtoto mdogo maziwa ya ng'ombe wakati bado anahitaji maziwa ya mama.
  5.   Kurithi.
Dalili za kisukari ni kama zilivyo katika makala yetu ya kwanza ila kuu zaidi ni hizi zifuatazo:-
  • Kukojoa mara kwa mara
  • Kiu ya mara kwa mara
  • Kuchoka mda wote
  • Mtoto kupungua uzito
  • Kupungua wa uelewa darasani
Dalalili hizi zinatokea haraka sana, Na endapo mtoto anapata mojawapo ya dalilii hizi basi mwahishe hospitali maana akizidi wiki moja bila tiba madhara makubwa yanatokea ikiwemo ubongo kudhurika na kifo.
Hawa watoto wanaweza ishi maisha marefu hata zaidi ya miaka 70 ikiwa masharti ya dawa na chakula yanafuatwa. Insulin,Lishe, mazoezi na kukubali hali hii, maisha yanakuwa bora na kuleta maana zaidi kwa mgonjwa yeyote wa kisukari.

Tusiwatenge wenye kisukari maana haiambukizwi na utendaji haupungui ikiwa masharti yanafuatwa ipasavyo.Dunia na nchi yetu zimebadili mtazamo na nia  katika ugonjwa wa kisukari. Miaka iliopita watoto wengi walifariki kutokana na kukosa insulin. 

Makamu wa rais alitangaza kwamba, Serikali yetu itajitolea katika kuwapa watoto insulin na vifaa vya kupimia. Na sisi katika jamii tunajukumu la kuwapenda na kuwatunza wagonjwa wakisukari. Tusiwatenge ni wenzetu katika maendeleo. Wengi wameishi na huu ugonjwa zaidi ya  mawazo na mitazamo ya wengi.
Picha uionayo hapa chini ni mtoto anaeishi na ugonjwa wa kisukari.


Jina limehifadhiwa.
No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda