Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Thursday, July 12, 2012

AFYA KWANZA: KUKABILIANA NA ULEMAVU WA VIUNGO

Na Bearice Githiri-HLH
Ulemavu wa viungo vya mwili hutokea pale ambapo mhusika anapungukiwa na uwezo wa kutumia viungo Fulani vya mwili kikamilifu kwa hali ya kawaida ya binadamu.
Hali hii inasababishwa na
Kuzaliwa hivyo
Ajali kwa mfano  kuanguka
Kuugua

Pasipo kuzingatia sababu ya huu ulemavu, kunauwezekano wa kutibu ulemavu aidha kikamilifu au kwa kiasi cha kuridhisha. Ikitegemea mhusika amefuata huduma hii kwa kuwahi ama amechelewa kwa kiasi gani.
Kwa suala la mtoto kuzaliwa akiwa na upungufu wa utumiaji wa viungo vya mwili, inakuwa ni changa moto kubainisha kama mtoto ameathirika mpaka pale ambapo kulingana na utaratibu wa kawaida wa kukua ( Developmental milestones), mtoto atahitaji kutumia kiungo fulani na awe ameshindwa.
Hii hali mara nyingi haitambuliki mpaka afikishe umri wa kati ya miezi sita na umri wa mwaka moja na nusu. Ni katika umri huu ambapo mtoto anaanza kufanikiwa kutumia viungo vyote vya mwili. Hapo ndipo anaketi, anatambaa, ananyanyuka na hatimaye kutembea. Pakitokea uchelewaji wowote kwa huu utaratibu, inapaswa mlezi wa mtoto mhusika kufuata huduma ya matibabu bila kuchelewa. Mtoto anavyozidi kucheleweshwa huduma ya matibabu ndo uwezekano wa kufanikisha hii huduma unadidimia.
Matibabu ya ulemavu
Kwa wale wanaopata ulemavu kutokana na ajali au kuugua, kuna taratibu mbalimbali za matibabu.
Cha msingi kabisa ni kutibu chanzo cha ule ulemavu. Kisha kuna maelekezo kupitia kwa waganga wenye taaluma ya mazoezi ya viungo kwamba ikitegemea kiasi cha kuathirika, mgonjwa anaweza akahudumiwa angali akiwa wodini au akahudhuria matibabu kama mgonjwa wa nje (OPD).
Haya maelekezo yanatofautiana kati ya mgonjwa mmoja na mwingine pia kati ya hali moja na nyingine. Kwa hivyo, ni muhimu sana kila mhusika apate maelezo kamili yanayomhusu yeye binafsi.
Ulemavu ukisababishwa na ajali mara nyingi huambatana na changamoto kadhaa kama vile vindoda. Hapo ndipo huduma ya matibabu inatolewa na wahusika wote tokea kwa daktari atakayekagua na kuelekeza jinsi ya kukitibu kile kidonda kwenda kwa nesi atakayesafisha na kukifunga kidonda, watunzaji washughulikie lishe bora na ikifikia kile kidonda kiwe katika hali ya kuridhisha ndipo mtaalamu wa viungo na mazoezi anahusishwa. Huduma inapotolewa katika mtiririko huu inakuwa kwamba hamna upande hata mmoja wa sekta za matibabu haujashughulikiwa kikamilifu.
Tukifuata haya yote kwa umakini, ulemavu unakuwa sio tishio kwa afya zetu kwani kulemaa sio hatima ya binadamu kuwa wa umuhimu kwenye ukuzaji wa uchumi wa mtu binafsi, jamii na taifa kwa ujumla.
Tusikate tamaa, tusichelewe tufuate huduma ya matitabu kwa muda unaofaa

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda