Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Friday, July 6, 2012

AFYA KWANZA: FAHAMU KUHUSU UGONJWA WA TB NA AINA ZAKE

Na Beatrice Githiri-HLH
TB ni ugonjwa sugu unaoambukizwa kwa njia ya hewa kupitia vinyelea vidogo ambavyo hatuweziviona kwa macho.

Aina za TB
1. TB ya mapafu
Aina hii ya Tb huadhiri mapafu na ndio inayowapata watu wengi. TB ya mapafu inaambukizwa.

2. TB isiyo ya mapafu
Aina hii ya TB huwa inaadhiri viungo tofauti na mapafu. Kwa mfano tezi, mzunguko wa tumbo na mapafu, uti wa mgongo, jointi, tumbo na njia ya uzazina mkojo hata na sehemuzingine za mwili.
 

TB inasambazwaje?
TB inaambukizwa kutokana na mtu aliye na ugonjwa wa TB haswa ya mapafu kupitia:
Ø      Kukohoa
Ø      Kupiga chafya
Ø      Kuongea kwa kukaribiana
Ø      Mate ovyo

Wadudu wakiwa wengi kwenye hewa, na mtu akiwa katika hali hio ya hewa ndio huchangia mtu kupata TB.
Hewa safi kwa kufungua madirisha na milango huzuia maambukizo.
Mwanga wa jua pia huua vinyelea  wa Tb lakini hawa wadudu  wanaweza kuishi kwa masaa 24-48 kwenye giza.

Dalili za TB ya mapafu
Ø      Kukuohoa mfululizo zaidi ya wiki 2
Ø      Makohozi yaliyochangamana na damu
Ø      Kuchoka, maumivu ya kifua, kukosa hamu ya kula,kupungua uzito, kupata homa usiku na jasho jingi

Dalili za TB isiyo ya mapafu
Ø     Maumivu ya kifua
Ø     Kuvimba tezi
Ø     Maumivu na kuvimba kwa jointi kwa TB ya jointi
Ø     Ulemavu wa uti wa mgongo
Ø     Kuumwa kichwa
Ø     Homa
Ø     Shingo kukakamaa na kuchanganyikiwa ikiwa ni Tb ya ubongo(menengitis)

Ikiwa mgonjwa na dalili zilizotajwa hapo juu ni muhimu kufika hospitalini kwa vipimo na matibabu.

Matibabu ya TB
Matibabu ya TB ni miezi miezi 6. baada ya wiki 2 za matibabu TB haiwezi ambukizwa. Ni muhimu kumaliza matibabu bila kuacha hata siku moja ili ugonjwa usirudi wala kukomaa.

Ushauri kuhusu ugonjwa wa TB
Ø      Unapoanza matibabu huwezi kuambuiza Tb tena.
Ø      Unaweza kupata TB kwa kuishi na mifugo nyumba moja ya kunywa maziwa ambayo hayajachemshwa au kula nyama mbIchi. HIvyo epuka haya mabo matatu.
Ø      Uonapo dalili za TB wahi hospitali kabla hujawaambukiza wengine.
Ø      Anika vyombo kwenye jua kuua wadudu wa TB.
Ø      Unapokohoa au kupiga chafya funika mdomo wako kwa kitambaa au ngu yako na sio mkono mkavu.
Ø      Pombe humaliza nguvu za dawa za TB hivyo acha kabisa ili upone.
Ø      Sigara inadhoofisha kifua chako hivyo huchochea kasi ya ugonjwa.
Ø      Matibabu ya TB ni bure hivyo usiogope gharama.


No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda