Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Tuesday, June 19, 2012

ZAKARIA ISAAY-KUUZA MAZAO MASHAMBANI NI KUUKARIBISHA UMASKINI
Na Mary Margwe,
Mbulu Manyara.
WANANCHI Wilayani Mbulu, Mkoani Manyara wametahadharishwa kuacha tabia ya kuuza mazao yakiwa mashambali hali inayosababisha upungufu mkubwa wa chakula Wilayani hapo badala yake amewasisitiza kukihifadhi chakula hicho kwa umakini pindi wanapokua wamekipata ili kiweze kuwasaidia.

Wito huo ulitolewa jana na Mwenyekiti wa CCM wilaya hiyo Bw.Paulo Zacharia Isaay wakati alipokuwa akizungumza na wananchi wa silaloda kwenye ziara yao ya kichama yenye lengo la kuhimiza uhai wa Chama  na maendeleo kiujumla.

Bw.Isaay ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo alisema kitendo cha kuuza chakula chote kikiwa mashambani  ni raha ya dakika moja na  ni shida na taabu ya mwaka mzima kwani kaya itakuwa imeingia katika umaskini usiotarajiwa.

Aliseama njaa inakwamisha shughuli mbalimbali za  kimaendeleo kwani  hakuna mtu yoyote atakayeweza kufanya kazi huku akiwa na njaa hivyo kila kaya ihakikishe kuwa inajiwekea akiba ya chakula cha kutosha kwa lengo la  kukabiliana na tatizo hilo .

“Hivi unafiki kuna mtu gani anayeweza kufanya kazi bila kula chakula, huku akifikiria nyumbani kwake hakuna chakul, huku anatakiwa kufanya kazi ya maendeleo labda huenda ni ujenzi wa shule ama kazi yoyote ile nani ataweza, hivyo unapolima mazao yako wakati wa kuvuna unaweka akiba ya kukusaidia baadaye na sio kuuza chote kule shambani “ alisema mwenyekiti huyo.

Aidha alisema wananchi wahifadhi chakula kwa ajili ya umuhimu wa maisha yao ili kuepukana na upungufu wa chakula utakaoweza kujitokeza, kwa kufanya hivyo kutawasaidia katika kuondokana na adha hiyo ya njaa.

“Hifadhini chakula  kwa umuhimu wa maisha yetu na familia zetu kwani mnapouza chakula chote tena kikiwa mashambani itakua ni raha ya dakika moja kwa kua umeiona hela na ni shida ya karibia mwaka mzima baada ya kuwa umemaliza zile hela, hivyo jaribuni pia kukumbuka kujiwekeaakiba yenu ya baadaye”alisema Bw.Isaay.

Aidha alisema hali ya njaa kwa Wilaya ya Mbulu haiko kwenye kata moja wala Kijiji kimoja bali karibia ni Wilaya nzima hususani kata ya Yaeda Chini wanakoishi wananchi wa jamii ya wahadzabe, hivyo ni vema wananchi wakajitahadhari kuhifadhi chakula mara wanapokua wamekipata, ambapo alisema serikali inafahamu hali halisi na italifanyia kazi suala hilo .

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda