Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Tuesday, June 26, 2012

Wananchi Hayderer walalamikia kuporwa kisha kutelekezwa kwa ekari 500 na DECOMNa Mary Margwe,
 Mbulu Manyara

Jumla ya ekari zipatazo 500 za Kijiji cha Hayderer kata ya Hayderer Wilayani Mbulu Mkoani Manyara zimedaiwa  kumilikishwa na uongozi wa Serikali ya Kijiji kwa kampuni ya DECOM na kuzitelekeza ekali hizo kwa kipindi cha zaidi ya miaka 30.

Hayo yalibainishwa jana na wananchi wa Kijiji hicho walipokua wakizungumza kwenye mkutano wa hadhara mbele ya Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM)  Wilayani hapo, Injinia Shekue Pashua, kitendo ambacho wananchi wamekemea na kulaani  vikali juu ya uroho unaofanywa na baadhi ya viongozi wa Serikali hiyo ya Kijiji.

 Wakiongea mbele ya Injinia Pashua, Wananchi hao wamedai kuwa kampuni hiyo inajishughulisha na shughuli za kilimo pamoja na uchimbaji wa visima vya maji ambapo makao yake makuu yako Mjini Arusha jamabo ambalo wananchi hao wameikemea na kulaani vikali kitendo cha uongozi wa Serikali ya Kijiji hicho kuimilikisha ardhi kampuni  hiyo na kuitelekeza kwa kipindi cha zaidi ya miaka 30 bila matumizi yoyote huku wananchi hao hususani vijana wakiwa wanakabiliwa na upungufu mkubwa wa maeneo  ya kilimo na mifugo.

Wakiongea kwa nyakati tofauti  kwenye mkutano huo wa hadhara uliofanyika katika kijiji hiko, wananchi hao walisema  kuwa shule ya sekondari ya Dongobesh iliyopo karibu na eneo hilo Wilayani Mbulu wameamua kuchukua ekari 50 kati ya hizo ekari 500 na hivyo kubaki 450.

 “Shule ya Sekondari ya Dongobesh tayari wenzetu wamechukua ekari 50  kutoka katika eneo hilo sasa sisi kama wananchi wa eneo hili tukisema tuchukue hatua kuchukua eneo letu tunaogopa vita watu wasije wakapoteza uhai na ndio maana tunaimba Chama na Serikali kuhakikisha mnachukua hatua kali za kisheria kwa mwekezaji huyo na kuturudishia eneo letu ili liweze kutunufaisha na si vinginevyo”alisema mmoja wa wananchi hao.

Kwa upande wake mzee maarufu wa Kijiji hicho Bw.Matheo Taric (85) alisema kuwa yeye anafahamu historia halisi ya eneo hilo kuwa lilikua lao kiasili, ambapo anashangazwa na uongozi wa Serikali ya Kijiji hicho kumilikisha ardhi kwa kampuni hiyo hatimaye  kuitelekeza kwa kipindi cha miaka hiyo bila mafanikio yoyote.

Bw.Taric alisema walau wangekua wamepewa na kulitumia walau hata watoto wao huenda wangepata hata vibarua katika eneo hilo kuliko kulitelekeza huku wananchi wakiangaika maeneo ya kilimo na mifugo.

 Alisema eneo hilo kwa sasa limekua tishio kwa watu na mifugo kwani kumekua na wanyama wakali kama fisi kwani mifugo yao mingi imekua ikichukuliwa  na wanyama hao wakali kutokana na pori kubwa jambo ambalo Serikali imetakiwa kuchukua hatua haraka ili kuweza kulinusuru eneo hilo.

“Sisi na watoto wetu tunakosa eneo la kulima na mifugo,wenzetu analiachia eneo kwa miaka 30 hivi kweli ni haki ya wapi jmani,katibu huwezi amini tunaumia na tumevumilia sana kwani toka enzi za Mbunge Marmo hadi sasa bado hatuja sikilizwa na kupatia ufumbuzi wa tatizo hili,sisi ni wazee sasa ambao tuna uvumilivu lakini kwa vijana wetu wa sasa hawana kabisa uvumilivu wanaweza kuchukua  hatua mbaya,hivyo naomba chana na Serikali mtusaidia kumaliza tatizo hili haraka”alisema Mzee Taric.

Akijibu hoja mbalimbali kuhusiana na tatizo hilo Katibu huyo Injinia Pashua alisema amesikitishwa sana na tatizo hilo  kwa kile alichokidai kuwa eneo hilo limekaa kwa muda mrefu bila mafanikio,jambo ambalo wangelimiki wangeweza kupata mafanikio mengi kupitia eneo hilo..

Aidha Injinia Pashua ameahidi  kulifuatilia suala hilo kwa  haraka kwa viongozi  ili kujua mikataba waliyowekeana  ili kuhakikisha kuwa eneo hilo linarudi kwa wananchi  na kugawiwa kwa wananchi mmoja mmoja  kwa wakazi wote wa Kijiji hicho ili waweze kunufaika nalo kisha ukaribu.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda