Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Wednesday, June 13, 2012

Wal-Mart, Pick n Pay moja wa wabia wa Alizeti Singida

Source: dewjiblog.com

Mwenyekiti wa SIFACU Omary Nyuda akifungua mkutano mkuu wa SIFACU uliofanyika kwenye ukumbi wa mkutano wa ofisi ya mkuu wa mkoa mjini Singida.
Msajiri wa vyama vya ushirika mkoa wa Singida Msafiri akitoa nasaha zake kwenye mkutano mkuu wa SIFACU.
Shamba la Alizeti.
Mafuta ya Alizeti yakiwa sokoni katika kituo kidogo ya mabasi yaendayo mikoa mbalimbali. (Picha zote na Nathaniel Limu).
Chama kikuu cha ushirika cha mkoa wa Singida (SIFACU LTD) kimefanikiwa kupata wabia mbali mbali watakaosaidia pamoja mambo mengine, kuboresha uzalishaji wa zao la alizeti na watakuwa wanunuzi wa uhakika wa zao hilo .
Mwenyekiti wa SIFACU Omary Nyuda wakati ametaja wabia hao na nchi zinakotoka makampuni hayo kwenye mabano, kuwa ni Fe-corporatin ( Canada ), Wal-mart (Afrika kusini), Pick N pay ( Japan ), Hans and Jhon Internationa ( Nigeria ) na Beijing Namo Tecti Trade ( China ).
Akifafanua amesema Hans and John International ya Nigeria , inatarajia kununua alizeti tani 5,000 kila mwezi.
Hata hivyo Nyuda amesema ili kumudu soko hilo la tani 5,000 za alizeti, vyama vya msingi vya ushirika vilivyoko chini ya SIFACU, vitalazimika kuomba kukopa kwenye taasisi za fedha, ili kuwa na mitaji ya uhakika.
Katika hatua nyingine, Mwenyekiti huyo almeakumbusha viongozi wa vyama vya msingi vya ushirika na wajumbe wa bodi ya SIFACU, kuwa ni nidhamu ya matumizi ya fedha, waadilifu katika shughuli zote za ushirika na kuzingatia kanuni zote za ununuzi wa mazao ikiwa ni pamoja na ubora, vipimo sahihi na utunzaji takwimu.
Kwa mujibu wa mwenyekiti huyo, alizeti ya mkoa ni ya asilia (Organic).
Msimu wa 2011/2012, mkoa wa Singida ambao unazalisha asilimia 60 ya alizeti nchini, uliuza nje ya mkoa zaidi ya tani 180,000 ambayo iliingizia mkoa pato ya zaidi ya shilingi bilioni 62.8.
SIFACU hadi sasa, ina vyama vya msingi vya ushirika 74.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda