Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Friday, June 15, 2012

Wakati wananchi wakitafakari Bajeti 2012/2013, HLH yapandisha gharama za matibabu

  • Zitaanza rasmi Julai Mosi
  • Ambulance sasa ni 10,000/= na kila kilometa ni 1,000
  • Kabla ya kutibiwa mgonjwa kulipia 20,000 kwa wakubwa na 10,000 kwa watoto
  • Wananchi wahoji uhalali wa kupandishwa kwa gharama hizo
  • Hatma ya wazee kutibiwa bure bada haijafahamika
Wakati serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia wizara ya fedha ikisoma makadirio ya mapato na matumizi (Bajeti) ya serikali kwa mwaka wa fedha 2012/2013, Hospitali ya Kilutheri ya Haydom (haydom Lutheran Hospital) imepandisha gharama za huduma hospitalini hapo zitakazoanza kutumika rasmi tarehe 1 Julai 2012.
Kwa mujibu wa matangazo yaliyobandikwa kwenye mbao za matangazo hospitalini hapo, gharama za kutumia gari la wagonjwa sasa zitakuwa TSh 10,000 ambazo hulipwa kabla na kisha kulipia Tsh 1,000/= kwa kila kilometa tofauti na awali ambapo mgonjwa hulipa gharama baada ya matibabu.
Aidha pia gharama za matibabu za wagonjwa wanaolazwa zimeongezeka ambapo wagonjwa wakubwa sasa watatakiwa kulipa TSH 20,000/= na watoto 10,000/= kabla ya matibabu na kama atakuwa ametumia gharama pungufu ya hela aliyolipa atarudishiwa fedha zake.
Mabadiliko haya yamekuja wakati wananchi mbalimbali hasa wa maeneo ya Haydom na vitongoji vyake wakihoji suala la wazee kutibiwa bure kama ilivyo kwa hospitali zote za serikali na zile zinazopokea ruzuku kutoka serikalini jambo ambalo halifanyiki katika hospitali hii ambayo kwa mujibu wa Makamu Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Mbulu ndugu Joseph Mandoo Guulo hupokea ruzuku ya zaidi ya shilingi Milioni 130 kwa kota moja (zaidi ya shilingi milioni 520 kwa mwaka) kutoka serikalini ili kugharimikia gharama za matibabu katika hospitali hii inayofadhiliwa kwa kiasi kikubwa kutoka nje hususani kutoka Norway.
"Hospitali ya Haydom inapewa ruzuku ya shilingi milioni 130 kwa kota na kwa mujibu wa taratibu wazee wote wanatakiwa kutibiwa bure, kama hilo halifanyiki hapo Haydom inabidi lifanyiwe kazi kwani hata katika kituo cha afya cha Bashay kilichopo chini ya kanisa Katoliki wazee hutibiwa bure" alisema Guulo
Hospitali ya Kilutheri ya haydom inahudumia jumla ya watu wanaofikia milioni 2 kwa mwaka kutoka katika mikoa ya Manyara, Singida, Arusha, Shinyanga na hata Dodoma huku ikitoa huduma za kliniki za kuwafikia watu vijijini (outreach) kwa kutumia magari na ndege. Kupanda kwa gharama za matibabu ni dhahiri kutawaathiri kwa kiasi kikubwa wananchi wengi ambao kwa hali yao ya kiuchumi ilivyo hawatamudu gharama hizo mpya za matibabu hivyo serikali kuombwa kuingilia kati kuwanusuru wananchi
"inaamaana kama sina 20,000 ndo sitapata matibabu"? alihoji moja wa wananchi ambaye hakutaka jina lake liandikwe. "Ugonjwa hautoi taarifa ili nijiandae kwa fedha, hii ndiyo "kwa sifa na utukufu" kama wanavyodai"?
Motto wa HLH toka mwaka 1967 ni "Kwa sifa na utukufu wake (To the Praise of His Glory" ambapo hospitali hii imekuwa ikitoa huduma kwa gharama za chini huku wafanyakazi wakilipwa mishahara kama ya serikali na pengine chini ya huo wa serikali japo ni si hospitali ya Umma huku wananchi wengine wakihoji uhalali wa kuongeza gharama hizo ilhali sehemu kubwa ya wafanyakazi kulipwa mishahara na serikali na pia ikipokea ruzuku toka serikalini.
Mwezi uliopita uongozi wa HLH ulipokutana na mbunge wa jimbo la Mbulu (CHADEMA) mheshimiwa Mustapha Akonaay waliiomba serikali iwaongezee ruzuku na kuanglaia upya sera ya kutoa ruzuku kupitia halmashauri ya wilaya ya Mbulu tu kwani Hospitali hii ipo katika mpaka wa wilaya tatu za Iramba, Hanang na Mbulu na ikiwahudumia wananchi wa mikoa ipatayo 5 na hivyo kubeba mzigo mzito wa gharama za kutoa huduma hospitalini hapo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda