Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Thursday, June 28, 2012

Wabunge 60 wajitokeza kupima UKIMWI na kutahiriwa

Na Seth Katende
Amini usiamini,
 Kampeni ya Kupunguza Ukimwi imewabidi wabunge wafanyiwe tohara na ni amri..Wote wenye mkono wa sweta lazima wapigwe mkasi fasta maana mkono wa sweta unachangia kuongeza maambukizi ya ngoma.

Kampeni hii inaendeshwa na Shirika la Population Services International na inaonekana so far wabunge wengi wamejitokeza kuitikia mwito wa kupima kwanza ngoma halafu wanaingia kupigwa mkasi fasta

Sipati picha hii ingekuwa Bongo hapa na hawa Wabunge wetu wabishi hawa, wangetoka nduki woteee Dodoma ingebaki nyeupeeee

Kampeni hii inafanyika Zimbabwe baada ya nchii hii kukumbwa na sakata la Maambukizi ya kufa mtu ambapo mwaka 2009 ilitangazwa kwamba asilimia 14 ya wananchi wa Zimbabwe wana waya,...Hatari

Kwa mujibu wa tamaduni za Zimbabwe Wanaume wengi huwa hawatahiriwi na hii imeonekana kuwa ni tatizo kubwa linalochangia maambukizi ya Ukimwi nchini humo


Mpaka kampeni hii inafanyika, watu wenye Ukimwi nchini Zimbabwe wanakisiwa kuwa milioni 1.1 na imebidi Raisi wa nchi hiyo, Robert Mugabe atangaze hadharani Mwezi March kuhusu hatua hii ikiwemo tangazo alilolitoa kwamba kuna marafiki zake waliokuwa wote kwenye chama walikufa kwa ugonjwa huo kwahiyo ni lazima hatua madhubuti zifanyike kuhakikisha wanapambana na ugonjwa huu!


Source: www.sethrhought.blogspot.com

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda