Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Thursday, June 21, 2012

Usiyoyafahamu Kuhusu Wadatooga: Ni mwiko kwa mwanamke kutaja jina la mkwe au hata jina linalofanana na la mkwe wake

Katika sehemu tatu zilizotangulia zinazohusu Historia, Maisha na Hatma ya Wadatooga kama jamii, tuliweza kupitia mambo mbalimbali kuhusu kabila hili ambalo limo hatarini kutoweka kabisa kama juhudi za makusudi hazitafanyika kuinusuru jamii hiiambayo imesambaa nchi nzima kwa ajili ya kutafuta malisho kwa ajili ya mifugo yao huku sehemu kubwa ya jamii hii ikimezwa kabisa na jirani zao yaani jamii ya Wairaqw ambapo zaidi ya 70% Wairaqw asili yao ni Wadatooga ukiwemo ukoo mkubwa kuliko wote wa Wairaqw wa Sulle, Hhay Tlawi na koo zingine nyingi.
Leo tutaangali Tabia, Miiko, Mavazi, Chakula na Nafasi ya Mwanamke katika Jamii

Tabia za Wadatooga

 • Ni wasema kweli na hawazunguki isipokuwa kwa mambo binafsi na kabila lake huwa wasiri sana (open, honest and straight forward)
 • Si waoga kwa jambo lolote (ni majasiri)
 • Wananidhamu ya hali ya juu kwa waliowazidi umri na hasa kwa wazee, akiagizwa hakuna kubisha wala mjadala
 • Wanaume wa kidatooga huishi katika nyumba yao inayoitwa "Hulanda" ambayo huwa mbele ya nyumba zote kwa ajili ya ulinzi wa familia na mifugo
 • Kutopenda kukaa karibu na wakulima na ndiyo maana Wairaqw waliweza kumiliki maeneo ambayo yalikuwa yanakaliwa na Wadatooga kwani Mwiraqw anapojenga karibu na Mdatooga, huyo mdatooga huhama eneo hilo
Miiko ya Wadatooga
 • Wadatooga hawali nyama ya nguruwe (hasa ngiri pori) na nyama ya punda
 • Jamii ya Barbayiga na Gisamjanga hawaoi wala kuolewa katika jamii ya Gidang`odiga (Karera) ambao ni Wadatooga wahunzi, japo wanashirikiana nao kibiashara
 • Mwanamke aliyeolewa ni mwiko kutaja jina la baba Mkwe wake au jina linalofanana na la mkwe wake
 • Mama wa Kidatooga haruhusiwi kuoga nje ya boma 
 • Mwanamke wa kidatooga haruhusiwi kutoka nje ya boma kama hajavaa Hanang`wenda (sketi ya ngozi anayovalishwa siku anaolewa kama ishara ya pete)
Mavazi ya Wanaume
Zamani Wanaume walijifunika migorori iliyotengenezwa kwa ngozi inayoitwa "Hangda badayda" na siku hizi hufunika mashuka. Jamii ya Buradida hujifunika mashuka yenye rangi nyeusi huku barbayiga wakijifunika mashuka yenye rangi nyekundu.

Mavazi ya Kike
Wanawake walioolewa wanavaa sketi ya ngozi (hata leo hii) ambayo ni ishara ya pete inayoitwa Hanang`wenda na kwa juu (top) wanavaa "aghwada badayda" huku wasichana wakivaa "aghawada badayda" tu

Chakula cha wadatooga
 1. Maziwa freshi ni kwa ajili ya watoto na wanaume huku wanawake na wasichana wanakunywa maziwa ya mgando
 2. Nyama: Wanaume wanakula nundu, ulimi, kidari na moyo wanawake wakila utumbo, maini na figo. Sehemu zingine wanakula wote
 3. Damu: Wadatooga hugema damu ya ng`ombe bila kumwua ng`ombe, damu hiyo hupikwa yenyewe au wakati mwingine hupikwa kwa kuchanganywa na unga kama ugali.
 4. Ugali: Kiasili wadatooga walikuwa hawatumii nafaka kama chakula ila siku hizi wanapika ugali wa mahindi, mtama na ulezi
Nafasi ya Mwanamke katika Jamii
Wanawake katika jamii hii hutegemewa sana hasa katika mauala ya maombi maarufu kama "ghaduweda" hasa yanapotokea majanga kama ukame, mafuriko, magonjwa ya mifugo, vifo visivyo vya kawaida au jambo lolote ambalo linahitaji "nguvu isiyo ya kibinadamu" kulitatua. (nitaeleza kuhusu ghaduweda katika makala nyingine)
Pia kama wanaume wameshindwa kutatua jambo lolote katika jamii, wanawake wa kidatooga wanauwezo wa kushinikiza mpaka utatuzi upatikane.No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda