Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Thursday, June 28, 2012

Ujumbe wa Pole kwa Dr. Ulimboka


Asalaam Aleykum wapenzi wasomaji wetu, ikiwa leo ni Alhamisi ambapo kama ilivyokuwa ada tunajadili kuhusu mada mada tete katika jamii yetu, leo sintofahamu ni kuhusu tukio la kusikitisha lililotokea juzi usiku la kutekwa na kisha kufanyiwa "uhayawani" na watu ambao hawana hata chembe ya utu kwa kumpiga, kumg`oa kucha na meno Dr Steven Ulimboka ambaye ni kiongozi wa Madaktari waliopo kwenye mgomo dhidi ya serikali wakiitaka serikali iboreshe mazingira yao ya kazi ikiwemo vifaa, madawa na malipo bora yanayoendana na hali halisi.
Wakati mgomo huo ukiiendelea juzi usiku habari zilienea kuwa Dr Ulimboka ametekwa na watu wasiojulikana waliojitambulisha kama askari na kutokomea naye kusikojulikana kabla ya kuokotwa kesho yake (tarehe 27 June 2012) asubuhi na "msamaria mwema" ambaye alitoa taarifa kituo cha polisi. Hali ya sintofahamu imeendelea kutanda miongoni mwa wananchi wengi ambao wamelihusisha tukio hilo na mgomo unaoendelea na kuacha hali kubwa ya Sintofahamu!

Kutokana na tukio hilo la kusikitisha, tunapenda kuwapa fursa wasomaji wetu popote ulimwengini kuacha ujumbe wa pole na kumtakia afya Dr. Ulimboka ili aweze kupona haraka na pia kulaani kitendo hichi cha kinyama. Ujumbe wako utachapishwa na pia utafikishwa kwa Dr. Ulimboka na familia yake ili kuwapa faraja kuwa tunawajali na tupo pamoja nao.
Acha ujumbe wako hapo chini katika sehemu iliyoandikwa "comments"  kwa kukibofya na kisha uandike ujumbe wako.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda