Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Thursday, June 7, 2012

Uga wa Teknolojia: Ujue mtandao wa kijamii wa Facebook

 Na Alexander Stephen-HLH
Mapema mwaka 2004 Mark Zuckeberg alianzisha Facebook ikiwa na URL ama anwani ya thefacebook.com, wakati huo Mark Zuckerberg alikuwa akisoma katika chuo kikuu cha Harvard huko Marekani
Jina la facebook(kitabu cha sura) lilikuja toka jarida ambalo vyuo vilipitisha kwa wanafunzi kila mwanzo wa mwaka ili kusaidia wanafunzi kufahamiana vizuri.
Facebook ilianzishwa kama njia kwa Mark zuckerberg na wenzake wa Havard kuwa karibu kimawailiano kwa kutumia mtandao wa internet na kufahamiana vizuri.
Mwishoni mwa mwaka uliofuata (2005) jarida hilo likafunguliwa kwa High Schools . Mwaka uliofuata tena (2006) facebook ikafunguliwa kwa jamii nzima lakini kwa sharti moja tu uwe na umri zaidi ya miaka 13.
Mark Zuckeberg
WAWEKEZAJI
Facebook ina wawekezaji wakiwemo, mwanzilishi wa PayPal bwana Peter Thiel, Accel Partners, na Greylock Partners. Mwaka 2007 Microsoft waliwekeza $ 246 milioni kwa hisa za asilimia 1.6%, mwezi uliofuat bilionea wa Hong Kong Li Ka – Shing aliwekeza pia kwa kiasi kikubwa sana.
Yahoo na Google walitaka kununua facebook lakini Mark Zuckerberg akasema Facebook haiuzwi.

FACEBOOK INAINGIZAJE PESA?
Kwa kiasi kikubwa Facebook inaingiza pesa kwa mapato yatokanyo na matangazo.
Ndio maana utaona Banners na Ads kwenye Facebook.
Hivo ndivyo wanavyowea kukupatia huduma hii kubwa kabisa bure.

Kwataarifa yako facebook ndiyo iliyo changia kwa kiasi kikubwa kwa kuondolewa madarakani kwa viongozi wengi wa mataifa ya kiarabu, wananchi waliitumia kama chombo cha mawasiliano kupanga maandamano na mambo mengine ya kimapinduzi.


No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda