Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Thursday, June 28, 2012

UCRT kuwawezesha wahadzabe kupata hati miliki za kimila ,sasa wamiliki ardhi yao


Na Mary Margwe,
Mbulu Manyara.

Wananchi wa jamii ya  wahadzabe wahishio katika bonde la Yaeda Chini Wilayani Mbulu Mkoani Manyara, wamekabidhiwa vyeti vya hati miliki za kimila ili kuiwezesha jamii hiyo kuweza kumiliki, kusimamia na hatimaye  kunufaika na ardhi  na rasilimali /maliasili  zilizopo  kwa lengo la kuinua hali ya kipato kwa jamii hiyo.

Jamii hiyo ambayo huishi kwa kutegemea kula mizizi, matunda, asali, ubuyu na nyama  kwa sasa imeanza kulala usingizi mnono mara baada ya shirika lisilo la Kiserikali la Ujamaa Community Resource Team (UCRT)  kwa kushirikiana na ofisi ya ardhi Wilaya imewawezesha hati miliki za kimila kwa Vijiji vitatu vya Yaeda chini, Mongo wa mono na Domanga.

Akikabidhi hati hizo, Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Bw.Anatory Choya  alilishukuru Shirika hilo la UCRT kwa jitihada za kuhakikisha kuwa wananchi wa bonde la Yaeda Chini wanakua na hati miliki za kimila kwani zitawasaidia katika kumiliki ardhi yao kihalali na huku wakiondokana na migogoro ambayo ingeweza kujitokeza hususani wanaovamia maeneo yao bila taratibu maalum.

Bw. Choya alisema changamoto kubwa iliyokua ikiwakabili jamii hiyo ya wahadzabe katika bonde hilo la Yaeda chini ni pamoja na uhamiaji holela wa watu kutoka nje ya Wilaya hiyo  na vijiji vya jirani ambapo kwa sasa tayari suala hilo limepatiwa ufumbuzi na  hilo shirika la UCRT.

Aidha alisema ni jukumu lao kuhakikisha kuwa hati hizo wanazihifadhi kikamilifu  na kuzilinda kwa umakini kwa ajili ya usalama wa mazingira yao wanayowazunguka, kwa kufanya hivyo kutawasaidia katika kumiliki ardhi yao kihalali, kwani umiliki wowote wa kitu unategmea zaidi kuwepo kwa hati halali  ya umiliki na si vinginevyo.

“Mara kwa mara kumekua na migongano juu ya ardhi, na sasa leo tunashuhudia UCRT na NDOROBO kutusaidia hati miliki za kimila zitakazowawezesha  kuondokana na kero ya mogogoro hii ya ardhi, kwani  kwa kazi hii mnayoifanya ni sawa na usuluhishi hivyo mnajitafutia baraka nyingi kwa jamii hii”alisema Mkuu huyo.

Kufuatia hilo aliitaka jamii hiyo pamoja na vijiji vilivyokabidhiwa hati hizo kuhakikisha kuwa hati  na uhifadhi wa mazingira  vinakwenda sambamba kama watoto mapacha kwa utunzaji wa mazingira kwani mazingira yakitunzwa ardhi itaimalika na huku itawajengea picha nzuri kwa waliowawezesha kupata hati hizo.

Kwa upande wake, Afisa miradi wa Shirika hilo Bw.Dismas Meitaya alisema Shirika hilo lilianzishwa mwaka 1998  likiwa na nia ya kuwaimarisha  jamii  za asili  zinazoishi  Kaskazini  mwa Tanzania  ikiwa ni pamoja na wahadzabe, waakie/ Ndorobo, wamasai, watatoga, na wasonjo(watemi) ili waweze kutunza, kunufaika  na kuendeleza rasilimali  za asili zinazopatikana kwenye mazingira yao  katika msingi enderevu.

Akielezea lengo kuu la Shirika hilo Bw.Meitaya  alisema ni kuhakikisha wanajenga uwezo wa jamii ya wawindaji na wakusanya matunda, wafugaji  na wakulima ili waweze kumiliki, kusimamia na kunufaika  na ardhi na rasilimali /maliasili zilizopo kwa hali ya kuinua maisha ya jamii hiyo na hatimate kupata kipato chenye tija.

 “Moja ya imani yetu  sisi kama Shirika la UCRT ni umiliki wa ardhi kijumuia kuwa ndio njia pekee ya kunusuru maisha ya wanyonge katika  matumizi  ya ardhi na kuheshimu  mila na desturi kuwa ni njia  sahihi ya kujenga utu wa binadamu” alisema Bw.Meitaya.

Akielezea baadhi ya mikakati ya UCRT  katika hatua ya kufikia lengo kuwa ni pamoja na kuiwezesha jamii kutambua haki zao juu ya arhi  na maliasili, kubainisha mipango ya matumizi bora ya ardhi kwa njia shirikishi, pamoja kushirikiana  na jamii kutatua migogoro ya matumizi ya adhi  na maliasili  kwa njia ya majadiliano.

Naye Afisa ardhi Wilaya Bw.Deogratius Mathia alisema hati zilizotolea ni 4 ambapo zote zilikua za maeneo ya kijamii, ambayo  yaliyotengwa kwa ajili ya malisho ya mifugo, hifadhi ya mistu/wanyamapori ya jamii katika  vijiji hivyo vitatu, Yaedachini hati 2, Mongo wa Mono hati moja na Domanga hati moja.

Bw.Mathia alisema utoaji wa hati miliki  hizo ni kuongeza usalama wa umiliki  na usimamizi  wa arhi hizo  kwa madhumuni ya  kuwa adhi  hiyo  itabaki na kulindwa  kwa matumizi ya malisho ya maifugo  na hifadhi ya jamii na hivyo kusaidia ardhi  hiyo kutovamiwa kwa ajili ya matumizi mengine  zaidi ya hayo.

Akizungumzia matarajio alisema kuwepo kwa matumizi ya maliasili zilizopo, kuongezeka kwa kipato  cha jamii kwa uuzwaji ya hewa ya ukaa(carbon dioside), ambapo alisema zoezi hilo la utoaji wa hati miliki za kimila  litakua endelevu kwani bado linaendelea kwa maengine  ya kajamii  yaliyotengwa  na huku wakiwa na mpango wa kuandaa hati miliki kimila kwa mwananchi mmoja mmoja.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda