Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Tuesday, June 12, 2012

Tumefika 10,000: Kwa pamoja tumeweza, tunasonga mbele na katu haturudi nyuma


Tulianza kama utani vile, mwezi moja uliopita ungeuliza ni lini ohayoda ingefikisha wasomaji hata 100 ilikuwa ni ndoto na haikuwezekana akilini kwa wengi hasa kutokana na kuwa ni jambo geni, lisilofahamika kwa wengi huku kwetu na pia ugumu wa kuweza kupata huduma ya internet na zaidi ya yote utayari wa wadau kutoa habari na kukubali kupigwa picha.
Fast Forward yaani peleka mbele haraka mwezi moja baadaye, hatimaye tumeweza kuvnja mwiko...safari iliyoanza kwa hatua moja tena kwa kuchechemea leo hii imefikisha hatua 10,000 na bado tunaendelea kusonga mbele....Kifuatacho? Hatua 100,000 na kisha 1,000,000...inawezekana na tutaweza
Tumekuwa tukipata maswali mengi kuhusu Jina Ohayoda na nichukue fursa hii kutoa maelezo ili kuondoa hii hali ya Sintofahamu; OHAYODA maana yake ya Jumla ni "Yowe" ama "Mbiu", Ukisema OHAYODA, OHAYODA, OHAYODA huku kwetu ni Yowe linapiga kwa Kupokezana, Ni Mbiu inayopigwa kwa kupokezana kutoka kwa Mtu mmoja kwenda kwa Mwingine. Blog hii ni Mbiu ambayo tunaipiga huku Kwetu Ili Kuvuta attension ya watu kuwa hata huku Kwetu kuna Utajiri Mkubwa, na kua mambo mazuri kutoka huku kwetu na sisi tumeanza Kupiga Mbiu hii Kuna Mwingine nae atatupokea kupiga mbiu hii pengine kuna Vijana wengine kama sisi Wataitikia Mbiu hii ya kwenda Kuendeleza Rasilimali zilizopo Vijijini.
 Timu nzima ya ohayoda inapenda kuwashukuru wasomaji wake woooote na wadau mbali mbali kwa mchango wao mkubwa usio na kifani ambao umetufikisha hapa tulipo. Wasomaji wetu wamekuwa mstari wa mbele kutupa mwongozo wa nini tukifanye ili hili libeneke liendelee kuwafaidisha wadau wengi zaidi.
Tutakuwa wachoyo wa shukrani kama walau tusipowashukuru baadhi ya watu na taasisi mbalimbali ambao wamekuwa na mchango mkubwa kutufikisha hapa tulipo leo. Kwanza kabisa ni Samuel Sasali aka papaa sebene ambaye amekuwa kichocheo kikubwa na kutoa mwongozo mkubwa katika kuanzisha blogu hii. Prosper Alfred Mwakitalima, Chris Mauki, Irene Lyatuu, Clara Kolle, James Temu, Protas Godwin na Anthony Luvanda na wadau wote wa Friends on Friday (FOF) ambao wametupa sapoti kubwa sana ya mawazo na critics na pia kuchukuliana nasi katika kipindi hiki tulipojichimbia Haydom na kukosa kushiriki shughuli za FOF
Beatrice Githiri mchango wako ni wa thamani sana kwa kutupa makala maridhawa ya afya kila ijumaa, Alex Steven Wambura wewe ni kichwa cha ukweli sana kwa kuwaelimisha wadau kuhusu mambo mbalimbali katika tekolojia ya habari na mawasiliano. Costas Onna mchango wako katika kutupatia habari na picha mbalimbali kutoka Mbulu ni wa thamani sana kwetu. Mungu awabariki kwa kujitoa kwenu japokuwa hampati kipato chochote kwa kazi yenu
Shukrani za pekee kwa Kituo cha Utamaduni Haydom (4CCP) kwa kutupa moyo na ushirikiano mkubwa sana wakiongozwa na mratibu wa 4CCP Anna Kari Evjen Olsen, mratibu msaidizi Eliminata Awet, katibu muhtasi Janeth John, mhifadhi wa nyumba ya makumbusho 4CCP Elfadhili Noah na wawezeshaji wa 4CCP Yakobo A. Massawe, Modesti Gilyo, Isaac Murge na Herman Malleyeck. Tunawashukuru sana
Mathew Mndeme "my invisible mentor", nakushukuru kwa mchango wako hata kama unaotoa kimyakimya, Marco Allute mfuatiliaji makini, Arthur Awet, Joachim John, Dr Edmond Lyatuu na Joseph Mandoo
Shukrani za pekee kwa Uongozi na wafanyakazi wa Hospitali ya Kilutheri Haydom, Chuo cha Uuguzi Haydom (HSN) ambao wamepokea ohayoda kama chombo chao, mali yao na sauti yao. Kuna wakati tuliandika habari nzuri na hata pale tulipoandika habari ambazo kimsingi hazikuwafurahisha walichukulia kama sehemu ya kujengana na kuboresha huduma katika taasisi hii iliyotukuka. Kwa uchache tunawashukuru Martha Massawe, Emmanuel Mighay, Barthlomayo Madangi, Mama Nakei na Paulo Tango Tunawashukuru sana kwa ushirikiano wenu mkubwa.
Shukrani Chama Cha Walimu Tanzania wilaya ya Mbulu, Idara ya ardhi ya wilaya na Gongali Development Model, Wasomaji wetu mahiri niwataje wachache: Wana Nyumbani Mbulu, Babati Forum na Karatu Youth News Club, Fakihi Fadhili Kakiva, Fadhili Magehema, Lilian Samuel, Dr Emmanuel Nuwas, Dr Joshua Gideon, Dr Fanuel Bellet, Henry Tlawi, Isaac Awaki, Augustine Namfua, Elifadhili Zebedayo Daudi, Elibariki Mushi, Afridenzi, Clement Daniel Paresso, Elisante Kebba, Goodluck Membi, Clodwig Basso, Emmanuel Elibariki, Robert Masanja, Zabroninho Vedastus, Edward Kibamba, George Martin Memba, Joycelyne John, Yotham Slaa, Askwar Hilonga na Edward Magessa.
Pachal Oswald na Dorothy Diella Ernest shukrani za pekee kwenu kwa kuwa sehemu ya kufanikisha ohayoda kufika hapa ilipo.
Wasomaji wa ohayoda, bila ninyi sisi tusingeweza kufika hapa tulipo. Mungu awabariki sana na tuzidi kuusambaza huu moto

Mwisho wa yote, Mungu akiwa upande wetu ni nani aliye juu yetu? Hata sasa Mungu ametusaidia

5 comments:

 1. Its all about movement for change ! kila la heri !

  ReplyDelete
 2. We don't aim for a change but for transformation....

  ReplyDelete
 3. In other hand we would love to thank you "Ohayoda " for the hard work you put into this blog...
  I know takes extreme amount of time and energy.

  We appreciate a lot. Keep doing what your doing ... "ohayoda " one of my favorite blogs.

  Ps .. I was so happy to see mum & dad in here the other day .. I haven't seen them in ages .. Special thanks for that :)

  Be blessed ...

  ReplyDelete
 4. Huwezi kuamini furaha na shukurani iliyojaa moyoni mwangu! Mungu akubariki Kiongozi wa OHAYODA, Amani Paul Gaseri, na wadau wote mnaohusika kwa namna moja ama nyingine. Sisi wana GONGALI MODEL tunaahidi kuendelea kutoa ushirikiano wetu katika hali njema na hata wakati wa wapungufu (for better or for worse)! Tupo pamoja!

  ReplyDelete
 5. Najisikia kushukuru tena na tena. Mungu azidi kuiongoza OHAYODA na ifikie malengo yake ya 100,000 then One Million,.... soon! Tutafurahi sana kusikia hilo lengo limefikiwa faster faster! STAY BLESSED!

  ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda