Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Thursday, June 7, 2012

SINTOFAHAMU: Ukweli kuhusu machimbo ya dhahabu, Gidurudagaw-Haydom

Mji wa Haydom ulivyokuwa kabla ya mgodi kuanza, sasa hivi unebadilika sana ndani ya miaka michache iliyopita
 Mu hali gani wapenzi wasomaji wa Ohayoda, kwa heshima na taadhima kama ilivyodesturi yetu kila siku ya Alhamisi tunatupia macho mambo mbalimbali yenye utata na kuzua walakini katika jamii yetu, mamb ambayo huzua maswali emngi pasipo majibu kutokana na ukweli kwamba huwa hayazungumzi waziwazi na hivyo kila mtu kuwa na jibu lake.
Leo baada ya kuandaa mada ambayo nilidhamiria kuiwasilisha kwenu ninyi wadau, mdau moja kupitia wa grupu la NYUMBANI MBULU kwenye mtandao wa kijanii wa facebook akaibua mada ambayo niliiona inamantiki tukiidadavua na kuijadili kwa pamoja.  Niweke wazi kuwa nitakayoyasema siyo hitimisho na kwa kuwa haya ni mambo ambayo hayana majibu rasmi, nitayaweka yote ili mwenye ufahamu ajaji yaani ahukumu mwenyewe lipi ni ukweli.
 Mada iliwasilishwa na Joseph Casmiri na hivi ndivyo ilivyokuwa 
Joseph Casmiri Habari wadau! Hivi yale madini yetu ya dhahabu kule haydom ilikuja kuwa vp tena naona no any activities tena! Tujuzane wenye info nn kilitokea tena??
Gerald German wazee wapiga kifafi kama unavyofahamu wazee wa iraq'w na wamang'ati wamefanya mambo yao ya kimila
Arthur Awet Jana tu kuna mtu alinidokeza habari hii, saying the same, wazee.........! duh! hi kali.
Gerald German ‎@Amani walifanya tambiko baada ya kuona girls & women are raped kisa ni machimbo hayo dont this anywhere ni hatari kwakweli
Yotham Slaa IT WAS SAID TO BE TRADITIONAL BELIEFS!BUT WHAT I CAN SAY IS THAT THERE WAS NO CLEAR INVESTIGATION WHICH HAVE BEEN DONE PRIOR TO MINERALS AVAILABILITY.TO KNOW WHETHER THERE WAS REALLY PRESENCE OF MINERALS!
Hayo ni maoni au mtazamo wa baadhi ya wadau wa mdahalo maarufu wa NYUMBANI MBULU, na ijulikane kuwa hawa wengi wao ni wasomi na wao kuwepo katika hali ya SINTOFAHAMU inaashiria giza totoro kwa wananchi wa kawaida.
Historia ya Machimbo?
Machimbo ya dhahabu ya Gidurudagaw yalipo takribani kilometa 8 kutoka Haydom yaligunduliwa katika miaka ya katikati ya 2000 ambapo yalivuta wachimbaji wadogowadogo kutoka sehemu mbalimbali nchini na kuchochea kasi ya ukuaji wa mji wa Haydom, ukuaji ulioendana sambamba na ongezeko la uhalifu, kupanda kwa gharama za maisha (mfumuko wa bei), mmomonyoko wa maadili ikiwepo kuongezeka kwa kasi ya maambukizi ya UKIMWI na zaidi uchafuzi wa mazingira hasa katika eneo la machimbo.
Akizungumza na Ohayoda, "Fadhili Saulo" ambaye alikuwa moja wa wataalamu waliokuwa katika uchunguzi wa awali (GeoChemical Suervey) yaani preliminary study katika eneo lote la ukanda wa Haydom kutoka kampuni ya Barrick Gold alisema kuwa uchunguzi wa awali ulionesha kuwa kulikuwa na dhahabu katika eneo hilo lakini kwa kiasi gani hakujua kwani mpaka anaacha kazi katika kampuni hiyo hatua ya pili ya uchunguzi wa kina ulikuwa bado na haijulikani kama uchunguzi ulifanyika tena au la.
Lakini taarifa zisizo rasmi zinadai kuwa Barrick Gold walifanya uchunguzi wa kina na kubaini kuwa hakuna dhahabu ya kutosha kwa ajili ya uwekezaji mkubwa na hivyo kutoa nafasi kwa wachimbaji wadogo kupewa vibali vya kuchimba katika eneo hilo. Hili lawezekana kuwa kweli kwani kama kungekuwa na deposit ya kutosha ya dhahabu kampuni ya Barrick katu isingeweza kuwaachia wachimbaji hao kuchimba madini hayo ukizingatia historia ya kampuni hiyo huko kanda ya ziwa. 
Uvamizi wa Wachimbaji wadogo
Baada ya kuruhusiwa wachimbaji wadogo ndipo kero zikaanza. Serikali kupitia vyombo husika haikuweka utaratibu mzuri wa jinsi uchimbaji ufanyike na nmna ya kuwaondoa wananchi waliokuwa wanaishi katika maeneo hayo ambao walionekana kuchukizwa sana na kitendo hicho kwani serikali ilitoa vibali kwa hao wachimbaji bila kuwapa maeneo huku ikiwaachia wachimbaji "wamalizane" na wamiliki. Wachimbaji hao walikuwa wanachimba ovyo pasipo kujali wanapochimba ni nyumbani, kaburi au shamba la mtu na wanapogundua kuna "mawe" ndipo wanamfuata mwenye eneo wamalizane! Mazingira yaliharibiwa sana na madini ya zebaki (mercury) yaliyotumika kusafisha dhahabu yalitapakaa katika eneo hilo, madini hayo ambayo ni sumu haijajulikana kama yalisababisha madhara ya kibinadamu.
Wakati yote hayo yakiendelea, serikali hasa Halmashauri ya wilaya ya Mbulu na serikali ya Kijiji cha Endaharghadatk wakati huo ilikuwa imekazia macho suala la mapato pasipo kujali maslahi ya wananchi ambao waliathirika siyo tu kupoteza maeneo yao bali hata kimaadili kwani yaliyokuwa yanatendeka huko hayakuwa ya kistaarabu.
Siku za mwanzo za machimbo hayo yalijaa neema kwa wachimbaji na hata watoa huduma hasa za maji na vyakula. Baadhi ya wenyeji "wajanja" waliwahi kushika mashimo na kuwakodishia wachimbaji wasiokuwa na mashimo. Aliyekuwa mchimbaji moja ambaye hakutaka kutaja jina lake anadai kuwa kipindi kile alikuwa na uhakika wa kupata hadi shilingi milioni 9 kwa siku. Jamaa huyu ambaye sasa hivi kafulia mbaya anaamini kuwa fedha zinazotokana na madini yale zimelaaniwa kwani hajui alizitumiaje na wala ziliishaje. Lakini uchunguzi mdogo ulibaini kuwa walikuwa na matumizi mabovu ya fedha kwa kuhonga wanawake, ulevi na kuishi maisha ya anasa na hawakuwa na utaratibu wa kuweka kumbukumbu , wahenga hawakuwa wajinga waliposema "mali bila daftari huisha bila habari" ati!
Je ni kweli wazee waliyapiga kifamfi?
Niliweza kuongea na moja wa waliokuwa wachimbaji ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa Kijiji cha Kidurudagaw (baada ya kujitenga kutoka Endaharghadatk) ndugu Hosea Gishinde kama kweli wazee "waliyapotezea mbali" kutokana na madhara ya kijanii yaliyokuwa yanasababishwa na uwepo wa machimbo hayo hapo, alinijibu huku akicheka kuwa "wazee walifanya mambo yao" na nilipozidi kumwuliza kwa nini anaamini hivyo alinijibu "hivi ndugu yangu unachimba sehemu unakuta linachangarawe kabisa na mawe mawe yakiwa yanaonesha mkondo wa dhahabu, unaweka alama lakini kesho unaporudi unakuta udongo mlainiiii hamna dalili ya mawe, sasa wewe hapo unadhani ni nini?"
Stori za namna hii ni nyingi sana mitaani na zinazidi kukolezwa na stori nyingine kuwa mzee anayehusika na tukio hilo ambaye sasa ni marehemu (jina limehifadhiwa) ambaye pia eneo lake ndilo lililoathiriwa kwa kiasi kikubwa na uvamizi huo, inasemekana huko miaka ya nyuma alikausha maji ya mto Gidurudagaw baada ya watu kutumia kigezo cha kunywesha mifugo katika mto huo unaopita karibu na shamba lake na badala yake kuchunga mazao yake akaamua kuyakausha maji ili isiwe tabu, na mpaka leo wananchi wa eneo hilo wanataabu kubwa ya maji maana hata kisima kilichochimbwa kilitoa maji mwanzoni lakini haijulikani maji yameenda wapi! Na ndo hivyo kasharudisha namba!
Baada ya mvutano baina ya wazee na wachimbaji, wazee hao wakaonekana kushindwa kuwazuia wachimbaji hao waliokuwa wanachimba kiholela, mfumuko wa bei ukawa wa kutisha kwani dumu moja la maji likawa linauzwa sh 2000 mgodini, nyumba za kulala wageni Haydom zikawa nyomi na kukawa na ongezeko la watu siyo machimboni tu bali hadi Haydom! Wachimbaji na hata wadau wengine wanaamini kuwa "mzee huyo" aliyapoteza hayo mawe ambayo uwepo wake maeneo mengi badala ya kusababisha neema yameleta maafa. 
Machimbo hayo hayakudumu kivile kwani wachimbaji moja moja walianza kuondoka mdogo mdogo, mawe yalianza kupungua na muda ulivyozidi kwenda idadi ya watu ikazidi kupungua hadi leo hii wapo wachimbaji wachache sana wenye "roho za paka" ambao wanaamini ipo siku mgodi utatema! Waliondoka wanaamini kuwa wazee waliyakausha na wanalaumu sana kuwa "wamewapotezea riziki zao"
Sintofamu, je ni kweli wazee waliyaficha hayo madini au ni kuwa hayakuwepo ya kutosha hivyo walipoyachimba waliyamaliza? yaani deposit ya dhahabu ilikuwa ndogo? Je kama kweli yalikwepo ya kutosha kwa nini Barrick Gold ambao ndio waliofanya utafiti wa awali hawakuamua kuyachimba? Au wazee hao walifanya "forecasting" wakawapoteza hadi Barrick? Mimi sintofahamu! Je haiwezekani kuwa wachimbaji hao waliamua kusema yamepotezwa kama maneno ya kujifariji wao kwa wao kutokana na ile hali ya kibinadamu ukishawekeza sehemu halafu ikala kwako? Hilo nalo lawezekana....maana ukiwauliza wachimbaji hao hawakuwa na taarifa zozote juu ya kiasi cha madini kilichokwepo na hata hakuna takwimu zinazoonesha kiwango cha uchimbaji kwa siku, kwani ukweli ni kwamba kila mgodi hujulikana unakiasi gani cha madini (deposit) na kwa kiwango cha uchimbaji wake uta"determine" yataisha baada ya muda gani
Mtazamo wangu: Kwanza niweke wazi kuwa binafsi hainiingii akilini kuendelea kuamini kuwa madini yalilogwa na wazee, tena katika karne ya leo. Tatizo ni kuwa watu wetu wengi hawapendi kutumia akili na huwa tunakimbilia kutoa "majibu rahisi kwa maswali magumu" na pengine kwa dunia ya sasa ni uwendawazimu kuamini kuwa bado mambo ya "kifamfi" yanafanya kazi. Ni imani potofu, na Sintofahamu imani hiyo itisha lini! 
Maandalizi mema ya weekend kesho! Ni hayo tu kwa leo. Kumradhi kuchelewa kuwaleta makala hii kutokana na sababu zisizoweza kuepukika
 

4 comments:

 1. Its myth, madini yapo ilavitendea kazi, na wote sasa wamehamia endabsh karatu (samunge)

  ReplyDelete
 2. duh nlijua Samunge ipo loliondo, kumbe Endabash napo

  ReplyDelete
 3. Ohayoda naomba utuwekee picha ya Haydom ilivyo sasa. Please ( only if you have time. Much appreciated )....

  ReplyDelete
 4. Jamani mtujuze kuhusu Dhahabu ya Masieda/Gunyoda.

  ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda