Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Thursday, June 21, 2012

SINTOFAHAMU: Hatma ya uwanja wa Mbulu Mjini

"Usiiondoe alama ya mpaka wa zamani, uliowekwa na baba zako" Mithali 22:28
Uwanja wa Mbulu Mjini
Sintofahamu ni makala inayokujia kila Alhamisi inayokupa fursa ya kuyafahamu mambo magumu ambayo majibu yake huwa hayatolewi na wahusika na hata pale yanapotolewa huwa ni majibu marahisi mno yasiyokidhi uhalisia wa hali ilivyo. Mada hii inadadavua mambo mbalimbali na kukupa uwezo wa kuyaona kwa jicho la tatu au kwa kiingereza wanasema "reading between the lines"
Leo SINTOFAHAMU ipo Mbulu mjini, mji ambao wajuvi wa mambo wanadai ulianzishwa siku moja na Nairobi lakini kama ilivyo kwa Mbuyu na Mchicha ambayo yote huanza sawa, leo haifananishwi! Tuachane na "hilo gepu" la Imboru na Nairobi, wiki kadhaa zilizopita Halmashauri ya wilaya ya Mbulu iliweka matangazo sehemu mbalimbali kuhusu ugawaji wa vibanda katika uwanja wa michezo uliopo eneo la Mbulu mjini. Wakati zoezi hilo likiwa bado laendelea na huku wadau mbalimbali wakitoa malalamiko yao "kichinichini" kuwa tayari vibanda hivyo vishawahiwa na "waheshimiwa" kama walivyofanya wakati wa ugawaji wa viwanja katika stendi ya Dongobesh ambapo inadaiwa "waheshimiwa madiwani" walijikatia keki wenyewe hali inayotia wasiwasi mkubwa wa kujirudi Mbulu mjini almaarufu kama "Imboru gera Guwangw"
Eneo la uwanja (nyuma-kushoto) ambako vibanda vilibomolewa
Tukiachana na hizo tetesi za waheshimiwa kutaka kuendelea kujimegea keki wenyewe, SINTOFAHAMU inaangalia uhalali wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu kuamua kuugawa uwanja huu wa michezo ili kuongeza vyanzo vya mapato kama inavyodaiwa.
Habari za kuaminika zinadai kuwa uwanja huu wa michezo ni mali ya Shule ya Msingi Hharka iliyopo hapo Mbulu mjini, uwanja ambao hutumiwa na wanafunzi pamoja na vijana kwa ajili ya michezo mbalimbali na kuwa Halmashauri haina uhalali wowote wa kukusanya mapato au kuugawa na kuufanya chanzo cha mapato badala yake wenye uhalali wa kufanya hivyo ni Shule ya Msingi Hharka ambao ndio wamiliki halali. Wiki kadhaa zilizopita vijana waliokuwa wanajitafutia riziki zao ambao wameamua kujiajiri wenyewe kwa kuuza nguo na viatu pembezoni mwa uwanja huo waliondolewa katika eneo hilo huku wakipewa masharti magumu ili waweze kupata vibanda katika eneo hilo litakapogawiwa ikiwa ni pamoja na kuwa na mtaji wa shilingi Milioni 5 ambao ni mkubwa sana kwa vijana hao.
Sintofahamu kwa nini vijana hao waliondolewa hapo, tetesi zinadai kuwa ni sababu za kisiasa zaidi kwani inasemekana vijana hao wamekuwa wakipeperusha bendera ya Chama ambacho kimeshinda ubunge katika eneo hilo, na huko nyuma wakati mbunge alipokuwa ametokea CCM walipeperusha bendera ya CCM na baada ya jimbo hilo kuchukuliwa na CHADEMA waliendeleza utaratibu wao kwa kuishusha bendera ya CCM na kuipandisha bendera ya CHADEMA. Wadadisi wa mambo wanadai kuwa, wakati kiongozi moja wa kitaifa alipofanya ziara Mbulu, baadhi ya vigogo wa CCM waliwaendea vijana hao wakiwaomba washushe bendera ya CHADEMA na kuiweka ya CCM japo kwa muda tu wakati kiongozi huyo anapita ombi lililokataliwa na vijana hao jambo lililopelekea viongozi hao kuapa kuwa vijana hao watajuta na hatma yake ndiyo hiyo kuondolewa katika eneo hilo.
Sintofahamu kwa nini Halmashauri iamue kugawa vibanda katika maeneo ambayo kimsingi na kisheria yanapaswa kuwa wazi hata kama wangekuwa na umiliki badala yake wangetafuta maeneo mengine yanayofaa kwa kazi hiyo. Maeneo ya wazi yanapaswa kuwa wazi kwa ajili ya michezo lakini kwa hili MDC linataka kuingia chaka.
Sintofahamu kwa nini shule ya msingi Hharka imekaa kimya, pengine ni kwa sababu mwalimu mkuu ni mwajiriwa wa Halmashauri hivyo anaogopa kitumbua chake kuingia mchanga, lakini je, i wapi bodi ya shule?  Wao ndio wenye maamuzi ya kugawa viwanja hivyo kwa waombaji ili kuwa chanzo cha mapato ya shule kama ilivyo kwa Shule ya Msingi Haydom ambayo imewapangishia watu mbalimbali viwanja katika eneo lake na kukusanya mapato kama mradi wa shule, na kama ilivyo kwa Chama Cha Mapinduzi Haydom ambayo imewapingisha wafanyabiashara mbalimbali katika maeneo yao na katu halmashauri haitii "pua" yao kutaka kukusanya mapato yasiyo halali yao.
Kwa leo sintofahamu halina la ziada, nilianza kwa kunukuu maneno ya kwenye Biblia kuwa usiondoe alama ya mipaka ya zamani iliyowekwa na baba zako, na hili lapaswa kuanzia kwa Halmashauri hii ya Wilaya ya Mbulu ambayo imekuwa Chanzo kikubwa cha migogoro ya Ardhi kwa kuwapora wananchi ardhi yao pasipo hata kuwapa fidia. Tutazungumzia kuhusu uwizi huu wa Halmashauri katika makala zijazo lakini Sintofahamu inapenda kutoa angalizo kuwa "Watanzania wa leo siyo wale wa mwaka 47, wanajua na wanachukua hatua"

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda