Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Wednesday, June 6, 2012

Shujaa Wetu: Askwar Hilonga na Gongali Development Model

"Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu" Efeso 3:20
Kila mtu yupo hapa duniani kwa makusudi maalum ambayo anatakiwa kuyatimiza kabla ya siku zak hazijakoma kuliona hili jua. Na hapa ndipo kasheshe linapokuja kwani usipojua kusudi lako hapa duniani utakuta unafanya kila kitu nusu nusu. Lakini yote katika yote, Mungu hutupa nguvu ya kuyatimiza makusudi hayo kama tukiamua kuyatimiza makusudi hayo na hapa ndipo tofauti baina ya watu huanza maana utakuta wote ni walimu au manesi au madaktari, wote mpo katika mazingira sawa na hata kipato sawa lakini moja anamafanikio zaidi na mwingine kila siku kulalamika au kulalamikiwa!
Askwar Hilonga
Kati ya watu ambao wameamua kulitumikia kusudi lao vyema kwa faida ya jamii kwa ujumla ni wanaharakati wa Gongali kupitia "Gongali Development Model" wanaoongozwa na Askwar Hilonga. Niliwahi kuandika siku za nyuma kuhusu Kijiji cha Gongali kilichopo Karatu jinsi kilivyokuwa chachu ya mabadiliko ya kisiasa nchini kwa kuwa kijiji cha kwanza kabisa nchini kumchagua mwenyekiti kutoka chama cha upizani mwaka 1994 (http://ohayoda.blogspot.com/2012/05/gongali-kijiji-cha-kwanza-tanzania.htmll) na Gongali bado inawasha moto wa mabadiliko ya kiuchumi nchini kupitia hizo harakati ambao malengo yao ni kutokomeza umaskini nchini ifikapo mwaka 2025.
Askwar Hilonga ambaye anashahada ya Uzamivu (PHD) kutoka Chuo Kikuu cha Hanyang, Korea na ni mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Nelson Mandela kilichopo arusha anasema kuwa PHD yake haina maana kama haitaweza kumsaidia kijana au mama aliyeko kijijini alikotoka au penginepo nchini ambao wapo katka wimbi zito la umaskini
Askwar na timu nzima ya Gongali Development model ambayo inaundwa na watu wa kada mbalimbali wakiwemo Mr. William Stephen Lohay, ALEX ATHANAS, Masozi Nyirenda,Yusuph Emanuel Tango na wengineo ambao wanajitolea pale walipo kuhakikisha kuwa wanapeleka miradi ya maendeleo vijijini na kwa kuwa wanatokea Gongali wameisaidia kwa kiasi kikubwa kijiji chao katika ujenzi wa shule ya msingi na miradi mengineyo.
"GDM ni harakati! Siyo msaada wala NGO, tunahitaji watu wajitolee (volunteers) kutoka kila pembe ya dunia ambao wanaamini katika tunayoyafanya na wapo tayari kushirikiana nasi kutimiza lengo hili kwa namna yoyote ile hata. Kama hao watakaojitolea watapenda kuja kufanya kazi Gongali kijijini, tutatoa huduma ya malazi bure. Tumekwisha kutoa kompyuta kwa shule nne za msingi za umma kutoka kwa Chuo Kikuu cha Hanyang-Korea lakini hazina walimu wa kompyuta, tumejenga shule ya sekondari, Benki ya Gongali (Gongali Microcredit Bank-GMC Bank) na huduma ya maji safi na maji taka inayofadhiliwa na Kanisa la Presbytarian la Korea na Kanisa la SDA linatoa huduma za Afya na huduma za kiroho. Kupitia harakati hizi, tunadhamiria kutoa mbinu 20 za namna umaskini unavyoweza kumalizwa Afrika. Tunakuomba uunge mkono hizi juhudi zetu uwe sehemu ya kampeni hii" Inasomeka sehemu hii kupitia tovuti yao ya www.gongalimodel.org
Shule ya Msingi Gonga
Siwezi kusema kama harakati hizi zitafanikiwa au la, lakini ni ukweli uliowazi kuwa hawa jamaa wamethubutu na mdogomdogo wameanza kupiga hatua pasipo kutegemea serikali wala misaada ya wazungu toka ulaya, wanajiwekea malengo na wanayatekeleza. Mungu alipomwita Musa awatoe Waisraeli toka utumwani Misri, Musa alidai kuwa hawezi kufanya hiyo kazi kwa kuwa yeye hawezi kuongea lakini Mungu akamwambia unanini mkononi? Musa akajibu anafimbo, na hiyo hiyo fimbo ndiyo iliyokuja kufanya ishara na miujiza mikubwa sana hata kupasua bahari ya Shamu. Gongali wametumia "fimbo" waliyonayo na ninaamini watafika mbali sana na kuwa mfano siyo tu Karatu na Tanzania bali hata ikawa mfano katika Bara la Afrika kuwa kijiji kimoja kidogo kilianzisha harakati za kuondoa umaskini Afrika kikafanikiwa badala ya kutegemea viongozi wetu wa kitaifa waende kutembeza vibakuli katika mikutano ya G-8 watuondolee umaskini lakini hali inazidi kuwa tete!
Unaweza kujua habari zaidi juu ya shughuli za GDM na hasa namna ya kuwa sehemu ya kampeni hii kwani Askwar anasema kampeni hii ni kwa ajili ya kila kijiji ambacho kitaona "approach" ya GDM inawafaa na hivyo kuibadili Gongali na kuweka jina la kijiji chao, mfano GDM kwa kijiji cha Gwandu Mehhi itakuwa Gwandu Mehhi Development Model..n.k. Tembelea tovuti yao www.gongalimodel.com
Ohayoda inawapongeza wadau wote wanaohusika na kampeni hii maridhawa ya Gongali ambayo inafaa kuwa mfano wa kuigwa na wasomi wote nchini hasa wa huku kwetu ambao wmekimbilia mijini na kuacha ndugu zao vijijini katika lindi la umaskini
Heshima Kwenu wana Gongali

2 comments:

  1. Shukrani mwandishi hodari sana Amani Paul Gaseri wa OHAYODA. Let's spread this candle fire EVERYWHERE, TO EVERYONE, EVERY-TIME, EVERY....

    ReplyDelete
  2. Tunashukuru sana mdau wa Ohayoda. Usiache kusoma libeneke hili nasi tutazidi kukupasha habari mbalimbali kutoka huku kwetu

    ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda