Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Monday, June 18, 2012

SHERIA NDOGO ZA MAMLAKA YA MJI WA MBULU.....SEHEMU YA KWANZA


SHERIA YA SERIKALI ZA MITAA, (NAMBA 7) YA 1982
(SURA 287)

KANUNI ZA KUDUMU

Zimetungwa chini ya kifungu cha 102

KANUNI ZA KUDUMU ZA MAMLAKA YA MJI MDOGO MBULU ZA MWAKA 2011
SEHEMU YA 1 
MASHARTI YA MWANZO

DIRA; Ni kuwa na Jamii inayopata mahitaji yake kwa viwango na yanayokidhi haki na usawa wa Binadamu ifikapo 2025.

NA KWA KUWA; Ni kuboresha utoaji wa huduma za Kijamii na Kiuchumi kwa kuzingatia matumizi yenye nidhamu kwa rasilimali zilizopo kwa kujali usawa baina ya Jamii.

NA KWA KUWA madhumuni ya Kanuni hizi za kudumu ni kuweka utaratibu wa namna Mamlaka itakavyoendesha mikutano na shughuli zake kwa kuzingatia misingi ya utawala bora:

SASA BASI, Kanuni hizi za Kudumu zinaelekeza ifuatavyo:

Jina na tarehe ya          1.       Kanuni hizi zitaitwa Kanuni za Kudumu za Mamlaka ya

Kuanza Kutumika          Mji Mdogo Mbulu na zitaanza kutumika mara baada ya

Kuidhinishwa na Mkuu wa Mkoa.

Tafsiri                    2.       Katika Kanuni hizi isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo:

Sheria Na. 7 ya 1982     Sheriamaana yake ni Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka

                                      za  / Wilaya) ya mwaka 1982;

Mwenyekiti

(a)          Kwa madhumuni ya Mamlaka ya Mji Mdogo maana yake ni Mwenyekiti wa Mamlaka ya Mji Mdogo Mbulu, Mamlaka ya Mji Mdogo na inajumuisha Makamu Mwenyekiti wakati anapotekeleza majukumu ya Mwenyekiti kwa mujibu wa Kanuni hizi;

(b)                         Kwa madhumuni ya Kamati, Bodi au Kamati Ndogo maana yake ni Mwenyekiti wa Kamati, Bodi au Kamati Ndogo;

Kamati:    

(a)          Inapotumika kuhusiana na Mamlaka ya Mji Mdogo ina maana ya Kamati iliyoanzishwa au iliyoteuliwa na Mamlaka ya Mji Mdogo chini ya Sheria;

(b)         Inapotumika kuhusiana na Kamati ya Maendeleo ya Kata ina maana ya Kamati hiyo;

(c)          Inapotumika kuhusiana na Kamati Ndogo maana yake ni Kamati Ndogo hiyo iliyoteuliwa na Kamati;

(d)         Inapotumika kuhusiana na Kamati nyingine ina maana ya Kamati hiyo;

Katibu” kwa maana ya Mikutano ya Mamlaka na Kamati zake ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Mji Mdogo au Afisa aliyeteuliwa kufanya shughuli za Afisa Mtendaji Mkuu wa Mji Mdogo.

“Mkurugenzi”           Maana yake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri au mtu yeyote aliyeteuliwa kufanya kazi za Mkurugenzi;“Afisa Mtendaji Mkuu wa Mji Mdogo” Maana yake ni Mtendaji Mkuu wa shughuli za Serikali katika Mamlaka ya Mji Mdogo na ni pamoja na Afisa yeyote wa umma atakayeteuliwa kutekeleza majukumu ya Afisa Mtendaji wa Mamlaka ya Mji Mdogo kwa mujibu wa Kanuni hizi.

“Mjumbe”               maana yake ni Mjumbe wa Mamlaka kama ilivyoanishwa kwa

mujibu wa Kifungu cha 45 cha Sheria;

          “Waziri”        Maana yake ni Waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa;

         

“Afisa wa Serikali za Mitaa” maana yake ni mtu ambaye ameajiriwa na au ambaye yumo katika Utumishi wa Mamlaka ya Serikali za Mitaa na ambaye anashika au anakaimu katika nafasi ya menejimenti.“Mamlaka ya Mji Mdogo” maana yake ni Mamlaka ya Mji Mdogo wa Mbulu ulioanzishwa chini ya Sheria Na. 7 ya mwaka 1982 Kifungu 13 cha Sheria hii.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda