Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Friday, June 29, 2012

Serikali kutumia nguvu Babati


Na Tabia Daffo, Babati.
SERIKALI wilayani Babati mkoani Manyara imesema ipo tayari kutumia nguvu endapo kundi la wavuvi zaidi ya 300 toka sehemu mbalimbali nchini waliovamia ziwa Burunge kwa shughuli za uvuvi haramu hawatatii sheria bila ya shuruti ya kurejea makwao
Kauli hiyo imetolewa juzi na mkuu wa wilaya hiyo Khalidi Mandia alipokuwa akizungumza na watendaji wa vijiji na kata katika mkutano wa kujadili udhibiti wa ujangili na ujirani mwema katika maeneo ya vijiji vinavyopakana na Hifadhi ya Taifa ya Tarangire
Akizungumzia sekta ya uvuvi hasa katika maziwa ya Babati na Burunge alisema imeshindwa kudhibiti ujangili dhidi ya samaki na mazali ya viumbe hai kwa kuwa kumekuwa na ubia kati ya watendaji wa serikali na wavuvi hao aidha pia rushwa ndogo ndogo imekuwa ikitawala miongoni mwao.
Akifafanua zaidi alisema kwasasa serikali iliyokuwa imeyafunga maziwa hayo tangu Januari Mosi mwaka huu hadi Julai mosi kupisha ongezeko la mazali na kukua kwa samaki imelazimika kuendelea kuyafunga maziwa hayo hadi Septemba mosi mwaka huu kupisha kukua kwa viumbe hai hao.
“tutapeleka boti ziwani na mtumbwi tutakaoutumia tutauchoma moto pamoja na nyavu haramu..najua viongozi na wananchi mtatuchukia kulifunga ziwa hili lakini hatuwezi kuvumilia kuona uharibifu huu uliosababishwa na kuacha kutii sheria zetu”
Aidha mkuu huyo alisema lazima viongozi hao kuacha kuwakumbatia makundi hayo na badala yake kuwaondoa kwa hiari vinginevyo serikali itatumia nguvu ya polisi kushirikiana kuwaondoa wavuvi hao ambao kwasasa wanakana kuendesha biashara hiyo kwa kujifanya kuwa wakulima ambao pia wamesababisha uharibifu wa mazingira na kutishia kutoweka kwa ziwa hilo.
Hata hivyo baadhi ya wavuvi waliozungumza na Nipashe walisema serikali haipaswi kuwaondoa kwa nguvu na badala yake ijaribu kutoa elimu kwao kwani wataelewa kama binadamu wengine lakini pia hatua ya kuwaondoa kwa nguvu kwa visingizio vya kuwatuhumu kuwa wakulima haina mantiki kwani wanayo haki ya kuishi hapo kama wananchi.
Kwa upande mwingine afisa mali asili toka idara ya wanyamapori wa halmashauri ya wilaya ya babati vijijini Nashon Maccokecha amekiri kuwepo kwa changamoto ya idadi kubwa ya wavuvi waliovamia ziwa hilo ambao wamekuwa wakitumia hila na ujanja wa kushirikiana na wenyeji hali ambayo inachangia uharibu na maangamizi ya viumbe hai ziwani humo
Alitaja changamoto nyingine inayokwamisha operesheni hiyo kuwa ni uhaba wa vitendea kazi ambao unawapa nafasi wavuvi hao kutumia magari na pikipiki kuwakwepa askari wa hifadhi hiyo kwa kuwa ziwa hilo lenye ukubwa km za mraba 40 limekuwa na forodha zaidi ya 10 na kushindwa kuwadhibiti.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda