Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Wednesday, June 13, 2012

Semina ya PETS yafungwa rasmi leo Haydom

Hatimaye ile semina ya Ufuatiliaji wa fedha za umma (Public Expenditure Tracking System) kwa ajili ya kuwafunza wenyeviti na maafisa watendaji wa vijiji na wanasheria wasaidizi (paralegals) kutoka vijiji 18 vya wilaya za Iramba, Hanang na Mbulu imemalizika rasmi leo majira ya saa saba mchana.
Kukamilika kwa semina hii kunafungua njia kwa uwazi na uwajibikaji kuanzia ngazi za chini za serikali nchini ambapo wanaporejea vijijini wanatakiwa kuunda kamati za PETS ambazo zitajumuisha watu 16 ambao watakuwa na jukumu la kufuatilia mapato na matumizi ya serikali.
Akizungumza na wanasemina, makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Mbulu ndugu Joeph Guulo Mandoo alisema kuwa atafikisha PETS kwa mkurugenzi wa wilaya ili kamati za PETS ziweze kutambuliwa na kupewa ushirikiano unaotakiwa ili wafanye shughuli zao bila kizuizi chochote na kuwataka viongozi wa vijiji kutokuogopa PETS na kuwaeleza kuwa uwepo wa PETS hauna nia ya kuwaharibia nia zao hasa kama wanafanya kazi zao kama inavyotakiwa.
Pamoja na semina kuhusu mfumo huu wa PETS, wanasemina walipata fursa ya kujifunza kuhusu VICOBA ambayo ilitolewa na Emmanuel Darabe na semina kuhusu mabadiliko ya hali ya nchi iliyofundishwa na Gilbert Mworia kutoka Norwegian Church Aid (NCA)
Katika muda wote wa siku 3 viongozi hao wa vijiji waliweza kujadiliana mambo mbalimbali ikiwemo kubadilishana mawazo baina yao wenyewe na pia na wakufunzi na kuahidi kuwa watarudi vijijini kuyafanyia kazi yote waliyoyajifunza na kuomba kuwa elimu waliyoipata ipelekwe pia kwa wananchi vijijini ili nao waweze kufaidika
Kituo chaUtamaduni cha Haydom (4CCP) imekuwa ikitoa mafunzo mbalimbali katika vijiji mbalimbali vya wilaya hizi tatu vikiwemo mafunzo ya Haki Ardi, VICOBA, Athari za pombe, Mabadiliko ya hali ya nchi na kufundisha kuhusu PETS.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda