Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Monday, June 11, 2012

Semina Ya Udhibiti wa Matumizi ya fedha za Umma (PETS) yafanyika Haydom

Kituo cha Utamaduni Haydom
Kituo cha Pembe Nne za Utamaduni cha Haydom (4CCP) ikishirikiana na Shirika la Misaada la Makanisa ya Norway (Norwegian Church Aid) inaendesha semina ya siku tatu inayoanza leo (inaendelea sasa hivi) ikiwashirikisha washiriki zaidi wa 100 inayowajumuisha wenyeviti na maafisa watendaji kutoka vijiji takriban 18 kutoka wilaya za Mbulu, Hanang na Iramba, wanasheria wasaidizi (paralegals) kutoka vijijini na wafanyakazi kutoka Haydom Lutheran Hospital (HLH)
Semina hii ambayo pia inahudhuriwa na Makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu ambaye ndiye alifungua, pamoja na kulenga kutoa elimu ya udhibiti wa matumizi ya Umma (Public Expenditures Tracking System-PETS) pia washiriki watajifunza kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa.
Wawezeshaji wa Semina hii ni ndugu Gilbert Mworia kutoka NCA Tanzania (Dar es Salaam) ambaye atafundisha kuhusu mabadiliko ya Hali ya Hewa na ndugu Emmanuel Darabe ambaye ni mwakilishi wa NCA Katesh ambaye anafundisha kuhusu Udhibiti wa Matumizi ya fedha za umma.
Awali akizungumza katika ufunguzi wa semina hii, ndugu Gilbert alisema nia ya semina hii ni kuhakikisha kuwa rasilimali za taifa zinatumika kwa faida ya wananchi na kuwa ufuatiliaji madhubuti wa utekelezaji na kutanabaisha kuwa wananchi ndio mabosi yaani waajiri wa viongozi walioko madarakani
Akifundisha kwenye semina hii, mwzeshaji Emmanuel Darabe alisema kuwa PTS ni mfumo au utaratibu wa wananchi wa kufuatilia mapato na matumizi na mapato ya fedha zinazotolewa na serikali kuu kupitia Halmashauri za wilaya hadi katika ngazi ya matumizi ya mwisho (vijiji na vitongoji).
PETS ni mfumo ulioanzishwa kwa sheria ya bunge ya mwaka 2007 na inawapa wananchi nguvu ya kudhibiti matumizi ya serikali ili kulinda haki na usawa na kusimamia rasilimali za nchi na kuepuka matumizi mabaya ya mamlaka. Malengo mengine ni
  • Kukuza uchumi na kupunguza umaskini wa kipato
  • Kuboresha maisha na ustawi wa jamii
  • kuhakikisha utawala bora na uwajibikaji
Aidha katika semina hii, washiriki ambao wengi wao ni viongozi wa vijiji walielekeza malalamiko yao kwa Halmashauri za wilaya zao kwamba hawapati 20% ya mapato yanayokusanywa katika vijiji vyao kwa mujibu wa sera
"Kijiji chetu kina mnada na halmashauri inakusanya ushuru lakini kwenye mnada lakini baada ya mnada wanatuachia uchafu" alisema Martini Akko ambaye ni mwenyekiti wa kijiji cha Endaharghadatk.
Mwenyekiti huyo aliendelea kufunguka kuwa mwaka 2001 Benki ya Maendeleo ya Afrika ilijenga mnada huo na wakaweka makubaliano na Halmashauri ya wilaya ya Mbulu kuwa 40% ya mapato ya ushuru yarudi kijijini hapo kwa ajili ya shughui za maendeleo lakini imekuwa kama ndoto za abunuasi.
Naye Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Mbulu na diwani wa kata ya Dinamu, ndugu Joseph Guulo Mandoo akijibu hoja mbalimbali za washiriki alisema kuwa ni kweli sera ya kurudisha 20% ya mapato kwa vijiji ipo lakini akakiri kuwa haijatekelezwa na imekuwa vigumu kutekelezwa.
Mandoo aliendelea kueleza kuwa halmashauri imekuwa na wakati mgumu wa kutekelezaji wa miradi mbalimbali kutokana na fedha kuchelewa kutoka serikali kuu (hazina) hali inayopelekea mwaka wa fedha kwisha na fedha kurejea hazina bila kufanya shughuli husika na hatimaye halmashauri kupata hati chafu
"Kama serikali kuu ingekuwa inaleta fedha kwa wakati na kukiwa na usimamizi mzuri nchi hii haina haja ya kutegemea misaada kutoka nje, mapato ya ndani yanajitosheleza kabisa" alisema ndugu Mandoo
Awali mweshaji Darabe alieleza kuwa mwaka 2010 halmashauri ya wilaya ya Mbulu ilipewa jumla ya Shilingi bilioni 19 lakini ikarudisha shilingi bilioni 2 hazina kwa kushindwa kuzitumia wakati kuna idara zingine zikitengewa kiasi kidogo kisichokidhi mahitaji
Semina hii imewaamsha washiriki ambao wameeleza kuwa PETS ni jambo zuri na wamehamasika kuianzisha vijijini mwao ili uwazi na uwajibikaji uanzie katika ngazi ya chini na kupendekeza kuwa ufanyike utaratibu ili hizi kamati za PETS ziweze kutambuliwa na uongozi wa halmashauri (wakurugenzi) ili wapate nguvu ya kufuatilia bila vikwazo.

Mengi kuhusu semina hii ya siku tatu yataendelea kuwajia live moja kwa moja kutoka kituo cha utamaduni cha Haydom (4CCP) ambao ndio waandaaji wa semina hii.

2 comments:

  1. EXCELLENT. Please see how you can bring this seminar to Gongali. WE NEED IT DESPERATELY! Thanks for your promise to bring more live reports....

    ReplyDelete
  2. Tanzania bila rushwa tutaweza? ??

    ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda