Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Tuesday, June 26, 2012

Papaa On Tuesday....Mti Ukikukinga na Mvua Leo Usiukate, Utakufaa Kesho


Na Samuel Sasali a.k.a Papaa 

Ninapenda kutuma Best Wishes kwa Wadau wa Blog Walio katika Mitihani ya UE kipindi hiki, maana utaratibu wa Siku hizi chini ya Tume Ya Vyuo Vikuu utadhani enzi zetu tunasoma Sekondari au Shule ya Msingi, Kama kufungua Wote ni tarehe zinazofanana na kama Kufunga wote ni tarehe zinazofanana, na Mitihani Wengi wanafanya tarehe zinazofanana, zangu Best Wishes Ziwafikie hapo mlipo.
Najua wengi wetu macho na masikio yetu yapo Dodoma kwenye kufatilia masuala mazima ya Bunge hasa kipindi hiki cha Bajeti najua wengi tunasikiliza Mstakabari wa yale yanayoendelea. Niliwahi kuandika juzi juzi hapa Kuwa Tanzania ni Kama Nyumba ya Mganga haiishiwi nyimbo ...http://samsasali.blogspot.com/2012/04/papaa-on-tuesdaynyumba-ya-mganga.html. Sasa hivi watu tumesha sahau kabisa habari ya Kesi ya Lulu, kuna Kawimbo kanakuja Ubeti wa pili kanaitwa "Mgomo Wa Madaktari" na Koras ya wimbo wa "Mgomo Wa Walimu" ikiwa inaendelea, angalau ule Wimbo wa Muungano ukaisha bila beti lake la mwisho kukamilika la kusema "Waislam Hawataki kuhesabiwa Sensa, Mpaka kipengere Cha udini kiongezwe", Maana Wiki iliyopita Kuna Single ilivuma sana ya Mhe, Mnyika ya Kusema eti hii nchi imefika hapa kutokana na "Baba etu Dhaifu" ilikuwa Single iliyopata wanunuzi wengi. Kwenye nchi hii nyimbo ni ngingi sana. Nasubiri kufanya Collection ya hizi nyimbo.

Kati ya misemo mingi ya Wahenga ninayoijua mmoja wapo ni huu wa "Mti Ukikufaa Leo Kijikinga na Mvua Usiukate, Utakufaa Kesho". Mara nyingi sana nimewahi wasikia watu wakisema hata mimi mwenyewe kuna wakati niliongea kuwa fulani ni mbaya sana, ama Ofisi fulani ni mbaya sana haina Maslah, au Mke wangu ama Mume wangu hafai kabisa, ama huyu ndugu yangu bureeee kabisa, tumekuwa ni wepesi wa kuponda vitu kwa Muonekano wa sasa na kudharau vitu vingi vilivyo sasa pasipo kuwaza miaka miachache ijayo kitu ama jambo hilo litakuaje.

Kuna watu wamekuwa wakidharau kazi wanazofanya sasa kwa sababu matarajio yao yako juu sana. walidhani mambo yatakuwa tambarare, baada ya muda wamekuja kugundua kuwa pengine wao ana yeye analipwa mshahara mdogo kuliko wengine, wanachofanya cha kwanza ni kuona kama kazi anayoifanya haina thamani ama yeye hana thamani, unajua unadharau leo mshahara ulio nao sababu upo, siku ukiwa hauna mshahara ndipo utakapojua thamani ya hizo unazoita senti zinathamani gani, wengi wanadharau kazi walizonazo sababu wanazo, waliokuwa na kazi ama shughuri ya kufanya wanajua thamani ya kazi hata kama ni ndogo kiasi gani, Kibaya Cha leo Kitunze, Kitakufaa Kesho.


Baadhi yetu tumekuwa na akili ya kudhani maisha ya Dar-es-salaam ni bora zaidi kuliko kule tuliko sisi, na kudharau rasilimali tulizonazo na kudhanganyika na watu wengi wanaovaa kwa kuchomekea na kwenda Saluni tukidhani maisha ya Dar-es-Salaam ni rahisi kiivyo, fursa za Dar-es-salaam ni Chache kuliko maelezo, Watu wachache wanamiliki taarifa za Jiji hili, rasilimali ni kugombania, ndio maana utaona Mtu anakaa Dar-es-Salaam, Ikifika Saa ya Kugombea Ubunge anaenda Kwaooooo, Kama Mjanja agombee hapa aone, hapa watu wanabanana, Usijidharau vile ulivyo ama pale ulipo, Biblia inasema utabarikiwa mjini utabarikiwa shambani kila mahali inahitaji kujipanga, Laini Laini Sio Rahisi Rahisi. Kila mtu kwa sasa Mjini anaamiki akitaka kufanikiwa mbali na kazi yake ni lazima Afuge ama Alime ndipo atakapofanikiwa, popote pale tulipo ni kujipanga, niliwahia andika kuhusu kujipanga gonga hapa...http://samsasali.blogspot.com/2012/01/papaa-on-tuesday-ukiona-mtu-anajipanga.html.

Kuna watu wana kawaida ya kuwadharau leo watu wanavyooonekana kwa maana kwenye akili zao wakiamini wale watu wataendelea kubaki kama walivyo. Kuna mdada alimpenda sana rafiki yangu mmoja, rafiki yangu alikuwa ana "m-feel" lakini alimuona sio type yake, kwa vile "hana mvuto" pamoja na kusihi sana lakini aliendelea ku mu-ignore kisa yeye anapenda Mke Matangazo, yaani anataka Comments za watu, tehe tehe unataka Mke Matangazo???basi Subiri, Jamaa akamuacha yule dada kwa maneno ya kejeri, mdada awa watu akaendelea na maisha Mungu sio Filikunjombe, mdada akapata zake kazi ya maana maisha yakamnyookea akaanza na biashara ghafla sura ya giza ikawa Nuru, baada ya miaka mitano wakakutana na Mkaka, na wakati huo Mkaka amechoka fulani na Mdada maisha yako level, Kijana akabaki tu kung'aa macho akajieleza weeeee, umewahi muona mwanaume akiwa amefanya kosa halafu bado anataka kujitetea kuwa alikuwa yuko sahihi hahaha  Kibaya Cha Leo Kitunze ndugu yangu, hakuna Mtu mbaya duniani ni matunzo, hakuna kazi mbaya duniani ni mtazamo, hakuna maamuzi mabaya ni Wakati tuu, uamuzi mbaya kuliko wote ni kuchagua Mauti wakati uliwekewa uzima mbele yako.

Kuna Wimbo unaosema "Wanaokudharau Siku Moja Watakusalimia Kwa Heshima", wengi tunadharau tulichonacho leo badala ya kukitunza, msema wa Kiswahili unasema "Kitunze Kidumu", huwa haijalishi sana watu wanakuonaje sasa ulivyo, Watu wanachukuliaje Makosa unayoyafanya, Watu Wanachukuliaje Machozi yako ya Sasa, Watu Wanachukuliaje Njaa yako ya Sasa, Stay Focus na Maisha yako, hakuna hali ambayo ni ya kudumu, Wanaojua historia ya Maisha yangu watakuambia, nimetoka mbali, Nimeuza Karanga, Ufuta, Maandazi pale Manzese Opposite na Friends Corner wakati tunaishi, tumeuza Ice Cream, Maji Baridi, nimewahi simamishwa shule sababu ya fujo, nikitazama nilikotoka na hiyo rough road hapo nyuma nabaki kusema "Yesu Ni Mwanaume". Rafiki yangu Prosper amewahi andika kwenye Facebook Wall yake " Every Saint has the Past, Every Sinner has the Future". Haijalishili unapitia nini kwa sasa lakini hii iwe ni kukutia moyo kuwa Unachokiona Sasa sio Cha Milele, Kama ni Kazi mbaya Si ya Milele usiidharau, Kama ni biashara usiidharau, kama ni mahusiano usiyadharau sababu kabla Daudi hajawa Mfalme alikuwa Mchunga Kondoo, na kabla Yusufu hajaingia Ikulu alikuwa gerezani, wiki chache zilizopita niliwahi andika, Siku Njema haziongozani gonga hapa....http://samsasali.blogspot.com/2012/02/papaa-on-tuesdaysiku-njema-haziongozani.html.

Siku zote Majuto ni Mjukuu, unaweza kumzuia Majuto kuwa mjukuu wako kwa kuamua kuwa na furaha kwenye maisha yako, amani ya Kristo na iamue ndani ya Maisha yako ya kila siku, Kama Ipo Ipo tu hata kama huioni....http://samsasali.blogspot.com/2010/12/papaa-on-tuesdaygods-ways-are.html.

Kibaya Cha Leo Kitunze, Kitakufaa Kesho, Mti ukikustiri na Mvua Usiukate Utamsaidia na Mwingine.

....//Papaa

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda