Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Tuesday, June 19, 2012

Papaa On Tuesday....Crabologous Behaviour Duniani Wapo Wengi Kukurudisha Nyuma

Mwaka 2011 tarehe 14 June, Niliandika hii Papaa On Tuesday inayohusianiana na "Elimu Ya Makaa". Tangu Mwaka umepita baada ya kuiandika wiki chache zilizopita nikiwa nasoma kitabu Cha Papaa On Tuesday Kitakachotoka hivi Punde, nikabaini kuwa Hawa Watu wa aina hii wanaumuhimu wake iwapo tu utachukulia mlengo chanya wa kile wanachokisema kwenye maisha, maana tangu nilipoanza kuandika na kupata Changamoto toka kwa watu wa aina hii nimekuwa imara imara zaidi ya kwanza.
 

Zangu salamu leo nazipeleka kwa wasomaji wangu walio kule hydom, maeneo ya Mbulu, Babati, Dongobesh na maeneo ya Jirani. Miaka michache iliyopita nakumbuka nilipita Kiteto nikaenda Mbulu, Kutoka Mbulu nilichukua landrover mpaka Dongobesh ambako nilifanya makazi yangu kwa Mchungaji wa KKKT Zakayo Malekwa. Ni safari yenye kukumbukwa sana. Siku chache zijazo nitakuwa huko Hydom kwa project mpya ya Blog nikishirikiana na Mwenyeji wangu Amani Paul Mzee Wa Kambi Popote.

Nianze kwa kusema Miaka Mingi iliyopita Evangelist Reinhard Bonnke aliwahi toa mfano wa "Elimu Ya Makaa" sijui kama ni Kiswahili Fasaha. Crabology ni muunganiko wa maneno mawili, Crab-Kaa (wale wa baharini) Logy inamaana ya "Elimu Ya". Crabology means the study of Crab(s) behaviors. Hawa watu wanasomea Elimu ya Kaa, wanasoma tabia za Kaa. Nilipokumbuka Mfano huu nikatafuta sifa mojawapo ya hawa Kaa. Nikapata maelezo yafuatayo.

Crabology (noun) : A needless effort to stifle others from succeeding [from the behaviour of crabs, when placed in a bucket, to stop each other from climbing out by pulling the other down back into the bucket]. Derived adjective: crabologous, crabologous behaviour (Submitted by: Huch from Texas on Feb. 24, 2007 06:14)
Katika maelezo haya ya Huch anaeleza kuwa ukichukua Kaa ukawaweka kwenye kapu kubwa hata ukikaa miaka mingapi ukija utawakuta wale kaa wapo mule mule. Katika kusoma kwake alibaini kuwa kaa ukiwaweka kwenye kapu, kama itatokea kaa mmoja akataka kutoka nje ya kapu, basi wale wale waliobaki wanamvuta tena arudi chini, yule aliyekuwa anamvuta mwenzake nae akitaka kutoka yule aliyemvuta nae anamvuta, miaka yote wanarudishana chini hakuna anayetoka nje wote wanabaki vile vile wanatamani wabaki kama walivyo hakuna anayeweza "kutoka" zaidi ya kutaka waendeleee na maisha yale yale wawe vile vile.
Katika maisha nimekutana na elimu hii mara nyingi, Crabology ipo mpaka kwa watu,yaani unapotaka kupiga hatua kutoka chini ya maisha yale ya kila siku kazi yao kubwa ni kukurudisha nyuma kukuvunja moyo, kukuambia hujui kufanya, kama unafanya unafanya vibaya,kwanza unafanya sio professional, ukiwaendekeza hawa "Crabology" inakula kwako. Kuna watu hawapendi kuona wenzao wanatoka nje ya Kapu la Maisha walilozoea kukaa.
Tangu nimeanza kufanya kazi za Blog, Presentations sasa hivi naelekea kwenye Productions ya Interview na Celebrates mengi nimekutana nayo. Kwenye kuishi kwangu na kazi hizi nimekutana na watu wa aina kuu tatu. Hata kwa sasa kwenye Project kubwa Ya Muziki wa Injili ninayoiingia chini ya Lebo Matata "Kiango" nimekutana na watu Wawili Watatu naona bado tuna changamoto.
Kundi la kwanza ni lile ambao linakukubali mpaka hawaoni ubaya wako wala makosa yako. Unajua mtu ukimpenda sana hata ubaya wake huuni. Upendo "Husitiri" wingi wa dhambi. Hawa ni kundi ambao kazi yao kubwa ni kukusababishia uone una "washabiki" watu wanakuunga mkono katika Jitihada zako za kimaendeleo. Hawa watu tangu zamani walikuwepo hawa ndio walioimba "Sauli Ameua Maelfu, Daudi ameua Makumi Elfu" hawa watu walikuza kichwa cha Daudi how is it Possible Daudi kumuua Goliath yamekuwa Makumi Elfu??hawa wanampenda Daudi. Ukiandika Papaa On Tuesday wao kazi yao kubwa ni Kutazama maana ya kile ulichoandika, hata kama umekosea wao wanaangalia ulichokuwa unataka kukumaanisha. Hawa watu wako upande wako kabisaaa. Hata kwenye makanisa hawa watu ni Zealots wa Mchungaji hata wakisikia Mchungaji wao anafanya uovu gani kwa sababu ya upendo wao wako tayari kufunika uovu huo. Hawa ni Wadau wako. Kwenye maisha una watu wanaokutazama very Positive hata ukipata tatizo gani wao wanamini ni bahati mbaya tu.

Kundi hili ni baya pia sababu halikuoneshi njia hata kama unakosea, hata kama watakusahihisha kwenye maisha mabadiliko kwao kama ni Option na sio kitu cha Lazima sana.
Kundi la Pili hawa wako 50-50 hawakukubali sana na wala hawakukatai sana. Hawa wanaangalia zaidi unakoelekea. Unapokosea kwenye kazi wanakuonesha tatizo na wanakuonesha Suluhisho la Tatizo. Nilipoanza kufanya Public Speaking, rafiki yangu mmoja aliniambia "Unafanya vizuri sana, lakini next time unatakiwa utumie practicle experiences zaidi kuliko mifano ya kufikirika". Kuna mwingine juzi kaniambia, Papaa Your doing a great Job ya Production, lakini unatakiwa next time usifanye moja, mbili, tatu" hawa wanataka uendelee kufanya kile kitu kwa usahihi zaidi. Wanatazama Production yangu ya 100 itakavyokuwa, lakini haiwezi kuwa nzuri kama ya kwanza kuna makosa nilifanya. Tofauti na group la kwanza wao wakiona Production wanabaki tu "Wow".

Kundi la tatu hawa ndo wale Crabologous yaani hawa wanaokatisha tamaa sana. Nakumbuka kuna mtu aliwahi nitumia email private, Blog yako inaboa sana, ina marangi rangi mengi, iko Unprofessional, unachelewa kubadili habari, hata unavyoandika andika mambo mengi yakufikirika zaidi hauna "Facts", hauna Reseach. Mwingine akasema Production zako ziko Poor, Location sijui imefanyaje, Camera unayotumia inaonekana ni kimeo, haamini kama Blog yangu inaweza kuwa hewani baada ya miaka kadhaa. Ukweli I was very disappointed sababu nafanya kazi silipwi na yeye nafanya kwa raha zangu lakini kunikatisha tamaa kwa kitu changu.
Kwenye maisha yetu ya kila siku lazima ujue unahitaji makundi yote matatu, na ujue kabisa Crabologous wapo wengi sana, wengine wanaweza kuwa ndugu zako wengine wanaweza kuwa rafiki zako wengine wanaweza kuwa hata hawakujui, kazi yao ni kuhakikisha haupigi hatua. Furaha yao ni kuona unaacha kufanya unachofanya, nia yao ni kukurudisha nyuma. Sifa kubwa ya watu wa namna hii Wao kuona Ubaya wako zaidi kuliko Uzuri wako. Na wao sio kwamba wanakitu wanafanya ila kazi yao ni kukutafutia Ubaya. Utasikia huwezi fanya sababu ya elimu yako, huwezi kufanya sababu Kinngereza Chako kiko Poor, Huwezi kufanya sababu hauko Professional, huwezi kufanya sababu wewe ni mwanamke. Ukiwaendekeza hawa utabaki kama ulivyo.
Ukikutana nao hawa watu, Chapa lapa watakusababisha ubaki kama ulivyo na itakula kwako.Kuna wakati inabidi ubaki na kile unachokiamini kuwa ndio ndoto yako, hata kama utakosea mara ngapi kama ndiyo ndoto yako usitegemee support kutoka kwa kila mtu kuna watu na viatu duniani watakukanyagia tu mahali fulani.Nirudie kusema hawa wa kukatisha tamaa wapo, ila chukua very positive ili uweze kupiga hatua dont get out from the game
....Papaa

+255 713 494110

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda