Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Monday, June 4, 2012

Njia Nyeupe: Ni Rahisi Sana Kutoka Kwenye Muungano


Na M. M MwanakijijiKuna maneno na kauli za baadhi ya watu wachache wakizungumza kana kwamba wanawakilisha “wengi”. Utasikia mtu anayepinga Muungano anasema “Wazanzibari hatuutaki Muungano” na wakati mwingine kudai “Wazanzibari wengi hawautaki Muungano”. Sasa mara nyingi wanaposema “wengi” mtu wa kawaida (asiyetaka kufikiri sana) anaweza kuamini kabisa kuwa ni kweli “wengi” hawautaki Muungano.
Mfano unaotolewa siku za hivi karibuni ni “sahihi 500,000″ za wanaodaiwa “Wazanzibari” wasiotaka Muungano. Sasa kwenye mahali ambapo pana watu milioni 1.5 hivi idadi hiyo ni kubwa sana; ni theluthi moja ya watu wote wa Zanzibar. Sasa kama kweli wapo watu wengi hivi njia rahisi ya kutaka kujitoa kutoka kwenye Muungano siyo mihadhara wala hawahitaji kabisa kuwalalamikia watu wa bara au serikali ya Muungano.
Kwa wanaokumbuka wananchi wa Zanzibar walishinikiza vyama vyao viwili vya CCM na CUF kuunda serikali ya umoja wa kitaifa na waliweza kufanya hivyo baada ya kupitisha sheria ya kura ya maoni ambayo hatimaye iliandika upya katiba ya Zanzibar. Wananchi wakaweza kujitokeza na kupiga kura ya maoni. Walifanya hivi bila kuomba kibali Muungano na kiasi cha kuweza kuandika kwenye Katiba yao vitu ambavyo ni kinyume na Katiba ya Muungano.
Sasa kama waliweza kufanya hili ni kitu gani kinawashinda kutaka viongozi wao wa kisiasa kuandika sheria ya kupiga kura ya maoni kama wanautaka Muungano au la? Kwa vile hoja ya kupinga Muungano inadaiwa inakubaliwa na watu wa vyama vyote ni wazi kuwa ni rahisi sana kwa watu wa Uamsho na Wazanzibari wengine kuhakikisha kuwa BLW linapokaa linaazimia kupitisha kura ya maoni kuhusu Muungano na kutaka sheria iletwe ya kuuliza swali la Muungano.
Swali liwe rahisi tu:
Je unataka Zanzibar ibakie kwenye Muungano wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania?
A. Ndio Ibakie – Ikibakia kero na matatizo ya Muungano kutatuliwa ifikapo Julai 1, 2014
B. Hapana Isibakie – isipobakia Zanzibar itajitoa ifikapo Julai 1, 2014
Ijulikane mapema kuwa ikisemwa kuwa “ndio ibakie” maanake ni kuwa masuala ya muundo na mfumo wa Muungano yatajadiiliwa na kushughulikiwa kwenye Katiba Mpya na yatakuwa tayari kumalizwa yote ifikapo 2014.
Na ikisemwa Hapana isibakie manae ni kuwa mazungumzo ya kuvunja Muungano yataanza na ifikapo Julai 1, 2014 Zanzibar itajitoa kwenye Muungano.
Wazanzibar waandae kura hiyo ya maoni wao wenyewe kama walivyofanya kwenye ile ya mabadiliko ya Katiba na lolote watakaloamua Tanzania Bara WATAHESHIMU uamuzi huo.
Ni rahisi sana kumaliza hoja ya kuwepo au kutokuwepo Muungano. Yote YAMO MIKONONI MWA WAZANZIBARI. Hawahitaji kutuambia hawautaki Muungano, hatuhitaji watuambie tunawakandamiza. Kama wanataka kutoka kweli na siyo mikwara mbuzi njia nyeupeeeee!! Andikeni sheria, itisheni kura ya maoni, pigeni kuchagua ‘B’ and then mambo yatakuwa yameiva ifikapo 2014 tutawasaidia kufunga

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda