Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Thursday, June 28, 2012

Mtandao wa ujangili wawahusisha watu maarufu na watumishi wa umma.Na Mary Margwe
Babati Manyara.

Imeelezwa kuwa mtandao wa ujangili  katika Mikoa ya kanda ya kaskazini umekua ni mkubwa huku ukiwahusisha baadhi ya watu maarufu nchini  pamoja na watumishi wa umma  wenye nyadhifa kubwa na hivyo kupelekea kuwa ni changamoto inayoikali Shirika la Hifadhi ya Taifa  Tanzania (TANAPA).

Hayo yalibainishwa jana na  Mhifadhi Mkuu wa TANAPA Mkoani Arusha ,Bw.John Shemkunde alipokua akiongea kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu  TANAPA  Bw.Allan  Kijazi, wakati alipokua akiwakilisha taarifa hiyo kwenye kamati ya ulinzi na usalama  za Mikoa ya Manyara,Arusha Kilimanjaro na Tanga (Kanda ya Kaskazini) ,kwenye ukumbi wa mikutano Ofisi ya Mkuu wa Mkuu wa Mkoa wa Manyara.

Alisema  licha ya kuwa Shirika la Hifadhi ya Taifa (TANAPA) kupewa dhamna ya kusimamia na kuendeleza maeneo yalioanzishwa kuwa hifadhi ya Taifa huku yakiwakilisha kiwango cha juu kabisa cha ulinzi  wa maliasili lakini bado baadhi ya watu maarufu  pamoja na watumishi umma  wenye nyadhifa kubwa  kuonekana kuwa tatizo kwani mtandao wao wa ujangili umekua ni mkubwa.

 Bw.Shemkunde alisema pamoja na kusisitiza dhana ya uhifadhi, shirika hilo  bado linajukumu la kuhakikisha kuwa uhifadhi huo unafaidisha wananchi kwa njia mbalimbali hususani utalii  na si vinginevyo .

“Mamlaka na dhana ya usimamizi wa hifadhi  za Taifa imeelezwa  katika sheria  za hifadhi za Taifa  sura namba 282 ya sheria za Tanzania ya 2002,ambapo shirika linatekeleza dhamana hiyo kwa kuanzisha na kusimamia kwa niaba ya wananchi, ni maeneo yanayojumuisha maliasili  na rasilimali  za kiutamaduni  ikiwa ni pamoja na mimea, wanyama, makazi ya  wanyamapori na maeneo  ya utamaduni  kwa ujumla” alisema Shemkunde.

Akizungumzia hali halisi ya ujangili  katika hifadhi  za Taifa Bw.Shemkunde alisema kwa ujumla  hali ya ujangili katika hifadhi za Taifa nchini  na maeneo mengine  yaliyohifadhiwa  imekua ni changamoto kubwa   kwa Shirika na Taifa  kwa ujumla, ambapo Shirika hilo limekua likijitahidi kudhibiti hali hiyo kwa kushirikiana na na wadau wengine ili kuhakikisha usalama wa maliasili  zilizopo katika maeneo hayo.

Aidha aliwataja baadhi ya wanyama  kama tembo ndio wanyama ambao wamekua  wakilengwa zaidi  na majangili  hao kwa sababu ya thamani  vipusa (meno yake) ambapo alisema faru nao wamekua wakishambuliwa pamoja na uchache wao, wamekua wakiwindwa sana kwa sababu ya upatikanaji  wa soko  la nyara zake katika baadhi ya nchi za huko Bara la Asia Uchina.

Akifafanua  alisema, jumla  ya majangili wapatao 4,021 walikamatwa kati ya kipindi cha mwaka 2009/2010 na 2011/2012  katika hifadhi za Arusha, Kilimanjaro, Mkomazi, Saadani, Tarangire na Ziwa Manyara ambapo alisema tatizo hilo kwa kiasi kikubwa linachangiwa na kukithiri kwa biashara ya meno ambayo mtandao wake umesambaa duniani kote kutokana na  kuendelea kuwepo kwa silaha zilizozagaa kiholela nchini .

“Kutokana  hasa na wakimbizi  kutoka nchi  jirani za Burundi  (DRC) Congo na Rwanda, pamoja na umilikaji wa magobore ambayo vibali vyake hutolewa na Halmashauri bila kuwa namna ya udhibiti wa kutosha ambako kunachangia kuongezeka kwa tatizo hili” alisema Shemkunde.

Akielezea mafanikio ya Shirika hilo alisema kuanzia 1959 hadi hivi Shirika limefanikiwa kuanzisha hifadhi za Taifa 15 na kuboresha majukumu yake ya uhifadhi kwa kujumuisha maeneo muhimu kwenye hifadhi za Taifa ikiwa ni pamoja na misitu ya asili kwenye hifadhi za Arusha,Kilimanjaro,na Ziwa Manyara.

“Maeneo haya yalijumuisha kwenye Hifadhi hizi ili mifumo ya kiokolojia na kuimarisha ulinzi wa misitu hiyo ambayo ilianza kuathirika  kwa matumizi  mabaya, Maeneo ya Usangu na Ihefu ambayo ni vyanzo vya maji muhimu kwa Taifa  nayo yalijumuishwa kwenye Hifadhi ya Ruaha na kuifanya kuwa Hifadhi  kubwa  zaidi  nchini na ya pili  katika  Afrika” aliongeza Shemkunde.

Hata hivyo alizitaja changamoto mbalimbali zinazoikabili Shirika hilo kuwa ni pamoja na ucheleweshaji wa hukumu za kesi  na adhabu zilizolingana(hafifu) na uzito wa makosa, umilikishwaji  wa bunduki za kuwindia (Riffles) uangaliwe upya kwani zimekua zikitumika katika ujangili  na uingizwaji holela wa silaha toka nchi jirani.

Aliongeza kwa kuwataka wadau wengine  kuwa na juhudi za pekee  hususani vyombo vya ulinzi na usalama vya mikoa yote minne inahitajika  ili kunusuru maliasili,na kuhakikisha kuwa changamoto zilizobainishwa zinapewa msukumo wa pekee ambao utatoa mafanikio na namna ya kupambana na ujangili huo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda