Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Wednesday, June 27, 2012


Mbunge wa Nyamagana (Chadema), Ezekia Wenje, akichangia bajeti ya Ofisi wa Waziri Mkuu bungeni jana
Mbunge wa Nyamagana (Chadema), Ezekia Wenje, amewashambulia wakuu wa mikoa waliokuja kusikiliza bajeti ya Ofisi wa Waziri Mkuu, na kudai kuwa ni matumizi mabaya ya fedha za serikali na wamekuja kula kiyoyozi bungeni.
Akichangia bajeti hiyo jana, Wenje alisema wakuu wa mikoa na makatibu tawala wa mikoa wamekuja na magari ambayo wanawekewa mafuta na wanapewa posho za kujikimu wakiwa Dodoma.
Alisema matumizi ya serikali bado ni tatizo na kwamba wakuu hao wa mikoa na makatibu tawala wamefika mkoani hapa tangu Jumamosi wiki iliyopita.
Alihoji kuwa wamekuja kufanya nini bungeni ama wamekuja kula viyoyozi katika sehemu ya Spika.
“Si hao tu; watakuja watu wa wizara ya ujenzi, watakuja watu wizara…wanakuja kufanya nini hapa? Wameacha kazi mikoani mwao, jaribuni kubadili mbinu hizi jamani,” alisema.

Wakati Wenje aliwalipua wakuu hao wa mikoa, kamera iliwaonyesha baadhi yao waliokuwa kwenye jukwaa la wageni wakionyesha mshangao kwa kauli hiyo

Source: www.ippmedia.com

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda