Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Tuesday, June 19, 2012

Madiwani watishia kuandamana hadi bungeni.

Na Mary Margwe,
Mbulu.
Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, Mkoani Manyara wametishia kuandamana hadi bungeni kwa kile walichikidai kulipwa  posho ndogo kulingana na kazi ngumu wanazofanya za kuharakisha maendeleo ya wananchi ambapo walidai kinyume na hivyo wataandamana kudai maslahi yao bungeni.

Wakiongea katika baraza la madiwani lililofayika jana katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, walisema posho ya sh.120,000 hailingani kabisa na shughuli za wanazosimamia na kudai kuwa haikidhi mahitaji yao na hivyo Serikali imeombwa kuwalipa sh.300,000 kama posho yao ya mwezi.

Akiongea wakati akifungua kikao cha baraza la madiwani, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Bw. Paulo Zacharia Isaay alisema madiwani wamekua wakilalamika mara kwa mara juu ya posho ndogo wanazopokea kwa mwezi, jambo ambalo wamedai wanaweza kuandamana nchi nzima, kama wanavyoandamaza madaktari, ama walimu ili kupata maslahi stahili.

Bw.Isaay alisema wakifanya hivyo kwa muda wa siku 3 huko mjini Dodoma lazima kitaeleweka, kwani watakapokua wamefika huko watalala kwa siku 3, huku wabunge na mawaziri watakua wamekosa sehemu za kulala na hatimaye kulala Morogoro kwani watakua wamejaza nafasi zote.

“Hivi unafikiri tukiandamana madiwani wa Tanzania nzima tukawahi kwenda Dodoma kama siku 2 kabla ya bunge kuanza, mwenye hali za juu wakawahi kulala zile hoteli kubwa kubwa na wengine wakalala hoteli za kawaida unafikiri wao watalala wapi kama si Morogoro, watakua wanatoka Morogoro na kuhudhuria Bunge Dodoma kwa siku zote hawataweza na tukifanya hivyo kwa siku tatu, lazima kitaeleweka na watatufikiria” alisema Bw.Isaay.

Aidha alifafanua kuwa kufanya hivyo, si kama watakua wanawakomoa wabunge ama mawaziri la hasha bali ni kuhakikisha kila mmoja analipwa stahili inayoendana na majukumu anayoyafanya  na si vinginevyo.

Mwenyekiti huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya hiyo, alisema licha ya kuwa wao wamebakiza miaka kama miwili kumaliza muda wao wa kuwatumikia wananchi, lakini zoezi hilo watalikuta madiwani wengine watakaofanikiwa kushika madaraka hayo.

“Tunajua kuwa kwa sasa imebaki kama miaka miwili tu kumaliza muda wetu kama madiwani,  lakini hata kama sisi tutaondoka basi wengine watakaokuja watanufaika na hii posho” alisema Mwenyekiti huyo.

Aidha alimtaka Mbunge wa Jimbo hilo Bw.Mustapha Akunaay kuhakikisha kuwa analipeleka tatizo hilo bungeni ili kupatiwa ufumbuzi wa mabadiliko hayo haraka iwezekanavyo ili kuweza kuwatia moyo madiwani katika hali ya utendaji wao wa kazi zao za kila siku.

Hata hivyo Bw.Akunaay alisema kuwa kilio chao amekisikia na atakiwakilisha katika sehemu husika kama lilivyomfikia.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda