Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Monday, June 4, 2012

Kutokana na chokochoko za Wazanzibari kutaka kujitenga, Je huu Muungano unamaslahi yoyote kwa Watanganyika?

Baada ya kushuhudia uvunjwaji mkubwa wa amani na kauli za kibaguzi za wazi kabisa kule Zanzibar dhidi ya Watanganyika wiki iliyopita, ikiwa ni pamoja na uchomwaji makanisa na uporaji wa maduka na baadaye kauli kutoka kwa kundi lingine likidai kuwa Wapemba waondoke Unguja na kuwa wao wanautaka Muungano jambo linalotimiza utabiri wa "mwenyeheri" Julius Nyerere kuwa ubaguzi ni kama dhambi ya kula mtu ukiianza katu hautaiacha kwani washaanza kubaguana kabla hata Muungano haujavunjika!
Wazanzibari wanadhani Watanganyika wanafaidika zaidi na Muungano, je ni kweli? Tanganyika itaathirika vipi na kuwa nje ya Muungano? Je Tanganyika imeathirika vipi na Burundi na Rwanda kuwa nje ya Tanganyika pamoja na kuwa sehemu yake wakati wa utawala wa Wajerumani? Kwani Zanzibar inatofauti gani na visiwa vya Ngazija (Comoros), Shelisheli (seychelles) na Mauritius? au hata Madagascar ambazo zote zipo kwenye bahari ya Hindi? Mbona tulituma majeshi kusaidia chokochoko Comoros? Je Watanganyika wenzangu mwasemaje? Na enyi Waunguja na Wapemba mwasemaje?

wiki hii Ohayoda inataka kupata maoni ya wasomaji kuhusu

Kutokana na chokochoko cha Wazanzibari kutaka kujitenga, Je huu Muungano unamaslahi yoyote kwa Watanganyika?

Jinsi ya kushiriki, piga kura kwa kuchagua maoni yako na kisha bonyeza VOTE juu kabisa upande wa kulia mwa blog hii na utaona kura yako inavyoongezeka na kubadili matokeo. Matokeo yatatolewa baada ya siku 7 bila uchakachuaji

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda