Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Wednesday, June 27, 2012

Tamko la Polisi kuhusu Dr. Ulimboka


Na Seth Katende, 
Dar es Salaam
Akizungumza na waandishi wa Habari Mchana huu, Kamanda wa polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, amesema Dk Ulimboka alitekwa na watu wasiojulikana akiwa Leaders Club akinywa pombe, pale Kinondoni


Kamanda Kova amesema Ulimboka aliokotwa na msamaria mwema ambaye hakutaka kumtaja jina lake kiusalama na kutoharibu upelelezo kuwa msamaria mwema huyo.Dokta Ulimboka aliokotwa katika msitu wa Mabwepande na msamaria mwema aliweza  kutoa taarifa kituo cha polisi cha Bunju, ambapo polisi aliyekuwa zamu alichukua maelezo yake na baadae Steven Ulimboka kuletwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili kwa matibabu zaidi.

Kamanda Kova amesema jeshi la Polisi Kanda Maalum limeunda jopo maalum kwa ajili ya uchunguzi na upelelezi wa tukio hilo la utekaji nyara, kwani ni tukio la kwanza kutoke nchini, ameongeza kwamba wahusika wote watakaobainika kuhusika na tukio hilo wachukuliwa hatua za kisheria na sheria itafuata mkondo wake ili kukomesha matukio mengine kama hayo


WAANDISHI WA HABARI WAKIMSIKILIZA KAMANDA KOVA
KAMANDA KOVA AKIONGEA NA WAANDISHI MCHANA HUU
Hii ndio hali ya dokta Ulimboka alipofikishwa Muhimbili Hospital.Inatisha aisee kama Tanzania tumefikia hali hii,amani iko wapi!
Dokta Ulimboka akionekana pichani wakati wakiwa kwenye mgomo wao wa mara ya kwanza na madaktari wenzake

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda