Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Tuesday, June 19, 2012

Kigogo wa CCM Dongobesh kizimbani kwa kutafuna posho za uchaguzi

Na Mary Margwe,
Mbulu Manyara

Katibu Kata wa  kata ya Dongobesh na  Gidhimu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilayani Mbulu,Mkoani Manyara Bw.Paulo Dayos amefikishwa katika mahakamani ya mwanzo ya Endagikot Wilayani hapo,  akituhumiwa kuiba sh.845,000 zilizotolewa na CCM kama posho za mabalozi wakati wa kampeni ya uchaguzi Mkuu uliofanyika mwaka 2010.

Akisoma shitaka hilo Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Mh,Rose Kisanga alisema kuwa kuwa mtuhumiwa Dayos alitenda kosa hilo Oktoba 26,2010 wakati wa uchaguzi Mkuu,ambapo alikabidhiwa kiasi hiko kwa ajili ya kuwalipa mabalozi wa nyumba kumi kumi ,ambapo alikula,na yuko  nje kwa dhamana hadi hapo kesi hiyo itakapotajwa tena Juni 18,mwaka huu.

“umefikishwa hapa kizimbani kwa kosa la wizi wa kuaminiwa ,ulikabidhiwa fedha ukawalipe nabalozi wa nyumba kumi na wewe ukaamua kuzila bila kuzifikisha,jambo ambalo ni kosa kisheria”alisema Hakimu Kisanga.

Wakiongea nje ya mahakama hiyo jana kwenye mkutano wa hadhara mbele ya Mwenyekiti wa CCM Mkoa  wa Manyara Bw.Lucas Ole Mukusi kuhusiana na tukio hilo, mabalozi hao wameuomba uongozi wa Chama cha Mapinduzi Wilaya kuhakikisha kuwa inawalipa fedha zao huku chama hiko kikiendelea na kesi hiyo inayomkabili Bw.Dayos.

Aidha mabalozi hao kwa sasa wameususia  uchaguzi wa mabalozi wa nyumba kumi kumi uliotakiwa kufanyika mwezi  februari mwaka huu,huku wakidai kuwa hawatafanya uchaguzi huo hadi hapo watakapokua wamepewa fedha hizo kama posho kwani ni  haki yao ya kimsingi.

Awali Mabalozi hao walisema kuwa waliposikia kuna posho itakayowafikia  ya sh.5000 kwa kila mmoja wao kati ya wabalozi wapatao 169 waliopo katika kata mbili  ya Dongobesh na Gidihim Wilayani hapo kutoka kwa Bw.Dayos, walifurahi kupita kiasi kwani wamedai haijawahi kutokea mabalozi hao kupatiwa fedha   kama posho.

Mmoja wa mabalozi hao alisema sio kama wao hawana hizo fedha la hasha isipokua wanadai kwa sababu ni haki yao halali ,hivyo ni vema wakapewa vinginevyo uchaguzi huo watausikia kwenye bomba.

Naye Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa  huo Bw.Flatey Glegory alisema kwa kua tayari kesi iko mahakamani hivyo ni vema wakavuta subira ili mtuhumiwa alipe hizo fedha mwenyewe badala ya chama kuwajibika kuwalipa mabalozi hao ,jambo ambalo lilipingwa na mabalozi hao wakidai wao kulipwa ndipo baadaye  chama kifuatilie hiyo kesi kwa wakati wao wakiwa tayari wameshalipwa posho zao.

“JAMANI sisi hatumjui huyo katibu aliyekula hela ,kama nyie mlimpa fedha alafu kwetu hajazifikisha sisi tutawadai nyie ndipo nyie mumdai huyo mtuhumiwa wenu,sisi tupeni chetu,kumbukeni sisi bado tunakipenda chama chetu cha CCM lakini baadhi ya watendaji wake wamekua waroho sana , yaani hawana uaminifu kabisa kwenye chama,hao wanatakiwa wawajibishwe kikamilifu ili wasirudie”alisema Bw.Peter Bariye

Hata hivyo kauli hivyo ilipingwa na Mwenyekiti huyo wa Mkoa Bw.Mukusi na kusema kuwa CCM Wilaya itawajibika kuwalipa mabalozi hao ,ndipo baadye iendelee kufuatilia kesi hiyo inayomkabili katibu kata huyo.

“Sumu ni sumu hata kama ni ndogo ,itaendelea kuitwa sumu tu na sio sumu ndogo,haki ni haki hakuna haki kubwa wala ndogo,jambo hata kama ni dogo ukizembea kulitatua mapema litakua kubwa na litaweza kukughalimu kwa kiasi kikubwa sana ,hivyo naomba msiwe na wasiwasi mimi nitahakikisha fedha hizo zinawafikia haraka ili kuweza kurudisha furaha yenu ya awali na kuendelea  kukipenda chama chenu cha CCM”alisema Mwenyekiti huyo .

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda