Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Monday, June 11, 2012

Inaendelea sasa hivi Haydom: Semina ya mfumo wa udhibiti wa matumizi ya fedha za Umma

Kituo cha Pembe Nne za Utamaduni cha Haydom (4CCP) ikishirikiana na Shirika la Misaada la Makanisa ya Norway (Norwegian Church Aid) inaendesha semina ya siku tatu inayoanza leo (inaendelea sasa hivi) ikiwashirikisha washiriki zaidi wa 100 inayowajumuisha wenyeviti na maafisa watendaji kutoka vijiji takriban 18 kutoka wilaya za Mbulu, Hanang na Iramba, wanasheria wasaidizi (paralegals) kutoka vijijini na wafanyakazi kutoka Haydom Lutheran Hospital (HLH)
Semina hii ambayo pia inahudhuriwa na Makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu ambaye ndiye alifungua, pamoja na kulenga kutoa elimu ya udhibiti wa matumizi ya Umma (Public Expenditures Tracking System-PETS) pia washiriki watajifunza kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa.
Wawezeshaji wa Semina hii ni ndugu Gilbert Mworia kutoka NCA Tanzania (Dar es Salaam) ambaye atafundisha kuhusu mabadiliko ya Hali ya Hewa na ndugu Emmanuel Darabe ambaye ni mwakilishi wa NCA Katesh ambaye anafundisha kuhusu Udhibiti wa Matumizi ya fedha za umma.
Awali akizungumza katika ufunguzi wa semina hii, ndugu Gilbert alisema nia ya semina hii ni kuhakikisha kuwa rasilimali za taifa zinatumika kwa faida ya wananchi na kuwa ufuatiliaji madhubuti wa utekelezaji na kutanabaisha kuwa wananchi ndio mabosi yaani waajiri wa viongozi walioko madarakani...
Habari zaidi na picha zitazidi kuwajia hivi punde................

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda