Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Thursday, June 21, 2012

Ijue Historia fupi ya Tovuti (Website)


Mu hali gani wapenzi wasomaji wa libeneke hili maridhawa la Ohayoda ambapo kama ilivyoada ya kila Alhamisi mtaalamu wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Bw. Alexander Stephen Wambura kutoka Haydom Lutheran Hospital anatujuza mambo mbalimbali katika uga huu wa TEKNOHAMA! Ungana na Alexander wakati anaelezea kuhusu historia fupi ya Tovuti au Website

Tovuti ni mkusanyiko wa kurasa zilizoandikwa kwa lugha mbalimbali za tarakilishi kama vile HTML, PHP, XHTML na kadhalika na ambazo kwa pamoja hujumuika katika kutoa habari au maelezo kuhusu jambo fulani. Lugha hizi, yaani HTML, PHP, XHTML na kadhalika zinaweza tu kusomwa na kutafsiriwa na programu kama vile Internet Explorer na Mozilla Firefox kwa lugha ambayo inaweza kueleweka na binadamu. Wingi wake ni "tovuti" vile vile. Tovuti zote pamoja zinaitwa "mtandao" au "Intaneti" au "wavuti".
Www (world wide web) ilitengenezwa mwaka 1990 na mwanafizikia wa CERN aliyejulikana kwa jina la Tim Berners Lee.
Mnamo tarehe 30 Aprili mwaka 1993, CERN ilitangaza kuwa world wide web itakuwa huru kwa matumizi ya mtu yeyote. Kabla ya kuanzishwa kwa html na http. Protokali zingine kama FTP na GP zilitumika kupata faili kutoka kwenye Server. Hizi protokali kaziyake ni kumpa mtumiaji mpanilio na muonekano mzuri ambao ataweza kupitia faili moja hadi lingine kwa urahisi zaidi, pamoja na ku download faili.
Kupitia website tunaweza kupata jumbe, matangazo na taarifa mbalimbali dunia nzima, makampuni pamoja na secta karibu zote za serikalini zinamiliki website ambazo hutumika kuweka matangazo na taarifa mbalimbali.
Kwa taarifa tu, kama utafahamu vizuri kutumia teknolojia hii unaweza kupata kufahamu bidhaa mpya zilizopo sokoni na kuzinunua moja kwa moja kupitia tovuti. Vyuo mbalimbali vya elimu ya juu, bodi ya mikopo, baraza la mitihani la taifa pamoja na Tume ya Vyuo Vikuu nchini.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda