Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Thursday, June 28, 2012

IJUE HAIBA YAKO (KNOW YOUR INBORN GOD GIVEN PERSONALITY)

Na Nelson Faustin
Ndugu wasomaji wa OHAYODA
Ni matumaini yangu kuwa mu wazima wa afya na Mungu wa mbinguni anawapigania kila uchwao.
Karibuni tujifunze kwa pamoja makundi makuu manne ya haiba za watu mbalimbali ili tuweze kuifanya dunia mahali bora pa kuishi.
Makala yetu itagawanyika katika sehemu mbali mbali ili kufahamu maana ya kila haiba, sifa njema (strengths) , madhaifu (weaknesses) na jinsi ya kuchukuliana na haiba husika.

Mungu ni wa ajabu sana kwani alihakikisha kuwa duniani patapendeza sana pakiwa na watu wenye tabia mbalimbali japo na uzuri au na mapungufu yao wote ni mali yake lakini ni jukumu la mwanadamu kujifahamu, kuwafahamu wanadamu wengine na kujua njia bora zaidi za kuishi nao, ili dunia aliyotupa tuweze kuiishi kwa amani, upendo, mshikamano na mafanikio zaidi na mwishoe tufike kwake mbinguni.

Ni vyema sana kuujua ukweli kuhusu kundi la haiba uliyo nayo hata kama huipendi kwani kwa kuufahamu ukweli utakuwa huru kweli kweli na utaweza kujikubali na kuishi na watu wote vizuri kwani jamii inabidi ione umuhimu wa uwepo wako  kwani ni wa thamani sana na utakuwa wa thamani zaidi kama utajifahamu vizuri.

Makala hii ni matokeo ya tafiti mbalimbali katika mitandao na walimu/wataalamu mbalimbali wa saikolojia, hivyo hata wewe msomaji wetu unaweza kuongeza ujuzi wako kwani hii ni sehemu ya kujifunza na kuelewa zaidi ya yale tunayoweza kuyapata darasani au katika jamii yetu. Kumbuka mazingira, malezi na maumbile yanaweza kubadili haiba Mungu alizotuumbia, makala hii itatusaidia kufahamu haiba zitokanazo na uumbaji ili tuweze kuishi sisi na si vile mazingira, maumbile au malezi yanavyoweza kutuumba.

Hivyo basi, kwa pamoja tutajifunza makundi yafuatayo:-
  • ·        SANGWINI-SANGUINE (sa’ng’gwin)
  • ·        MELANKOLI-MELANCHOLY (me’len-ko`l)
  • ·         KOLERIKI-CHOLERIC (ko`le`rik’)
  • ·        FLEGMATIKI-PHLEGMATIC (fle’g-mat`ik)
Tuonane kipindi kijacho siku ya jumatatu hapa hapa OHAYODA……………………………………………………….

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda