Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Friday, June 22, 2012

Hisia za Wananchi baada ya John Mnyika kutolewa bungeni kwa kusema "rais ni dhaifu"

Baada ya mbunge wa Ubungo mheshimiwa John Mnyika kutolewa bungeni baada ya kukataa kuifuta kauli yake kuwa "Tumefika hapa kwa sababu ya udhaifu wa Rais Kikwete, kwa uzembe wa Bunge, na kwa sababu ya upuuzi wa CCM na wabunge wake", ohayoda ilitaka kupata maoni ya wadau mbalimbali kuhusu hatua hiyo iliyochukuliwa na naibu spika dhidi ya mbunge huyo kijana wa chama kinachokutumia kauli mbiu ya "vua gamba vaa gwanda".
Yafuatayo ni maoni ya wadau hao waliyoyatoa kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii
Aidha wadau wengine wametoa maoni yao kupitia kura ya maoni inayoendelea kuendeshwa na Ohayoda ambapo mpaka sasa 95% wanasema Mnyika ni jasiri huku 5% tu ikidai kuwa ni mtovu wa nidhamu. Unaweza kuendelea kupiga kura yako kwa kchagua jibu sahihi kwako kisha bonyeza VOTE juu kabisa upande wa kulia mwa blog hii na utaona kura yako ikiongezeka bila uchakachuzi wowote na matokeo ya mwisho yatatangazwa hapa hapa tarehe 27/06/2012
 • Gerald German Huyo jembe jasiri sana kaongea ukweli mtupu
  Wednesday at 5:22pm via mobile · 

 • Philipo Paresso Mbunge makini sana,alichosema ni ukweli usiokuwa na shaka hata kidogo.
  Wednesday at 7:15pm via mobile · 

 • John Bura ni jasiri na ndo watu tunaowahitaji ktk kubadilisha nchi wanaosema ni utovu wa nidhamu ni fikra zao. Naona alisema kauli ya kawaida na yenye changamoto kwa rais. Kauli zili changamoto narudia kusema tena ili udhaifu ufanyiwe kazi. Mnyika angeulizwa kuwa udhaifu wa jk uko wapi angebainisha ili jk atake action on it. Tatizo letu waafrika hatukubali changamoto ndo maana tuko nyuma kimaendeleo. Mnyika hajaonyesha dharau hata kidogo ila alimpa changamoto jk. Tumeelewana jamani!
  Wednesday at 7:50pm via mobile ·  · 1

 • Godluck Lago J Mnyika ni jasiri sn wala siyo utovu wa nidhamu!!!!!!!!!!!!

   • Nicholaus Abdon naenjoy kuangalia mabunge ya kenya maana kumwambia mtu mdhaifu si tusi, David Cameroun kwenye bunge mananeno wanayomwambia kwenye maswali ya majibu, utamuona huyu hana kosa kabisa
    Emmanuel Tesha Mnyika kasema ukweli ktkt ya waongo wengi(CCM);Kaonyesha ujasiri wa hali ya juu mno kwakusimamia ukweli aliousema bungeni pamoja na kutakiwa kufuta kauli yake.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda