Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Tuesday, June 5, 2012

Hii haijakaa vizuri: Kubeba maiti hadharani

Emmanuel Mighay, Muuguzi Mkuu HLH
Sifa moja ya binadamu ni kuwa na utashi na ustaarabu katika mambo mbalimbali tofauti na wanyama au viumbe wengine. Kwaya moja miaka ya 1990 iliyokuwa inaitwa Barabara ya 13 Ulyankulu, Tabora waliwahi kuimba kuwa "Katika viumbe vyote vilivyoumbwa binadamu kaumbika kuliko vyote", na kuumbika huko siyo kwa hali ya muonekano bali hata ule utashi ambao unatutofautisha na wanyama wengine yaani utashi wa kujua jema na baya,
Kuna jambo ambalo nimekuwa nikilishuhudia mara kadhaa hasa maeneo ya hapa Haydom na leo nimelishuhudia tena na pengine si vizuri kama jamii tukalikalia kimya bali hatua madhubuti zikachukuliwa ili walau tuheshimu utu wa mwanadamu. Sijui wengine wanalichukuliaje lakini kwangu mimi na hata mashuhuda wenzangu leo walichwa vinywa wazi wasiamini wanachokiona pale ambao "ndugu wa marehemu mmoja" wapatao 4 walipoamua kuuchukua mwili wa mpendwa wao kutoka chumba cha kuhifadhia maiti cha HLH mchana kweupe (majira ya saa 7) bila kuwekwa hata kwenye jeneza na kumbeba hadharani na kuelekea kwenye makaburi kwa mazishi huku kukiwa na watoto wadogo na halaiki ya watu wakishuhudia kitendo kizima. Ninaposema hadharani namaanisha waliubeba mwili huo kwa kutumia mikono na kutembea nao kuelekea makaburini.
Mara kadhaa nimekutana na watu wakibeba maiti (hasa za watoto wadogo) na kwendaa kuwazika makaburini. Ni kweli kabisa yawezekana hawa "ndugu" labda si wenyeji wa hapa na pengine hawana uwezo wa kuwapa hao wapendwa wao pumziko linalomstahili binadamu yeyote lakini nadhani ni wakati muafaka kwa sisi kama jamii kuliangalia kwa jicho la kibinadamu suala hili kwani kwa kweli si ubinadamu hata kidogo.
Sitaki kuzungumzia kama kuna makosa ya kiutaratibu yaliyofanyika kuruhusu maiti hiyo itolewe kwani linafanyiwa kazi na uongozi wa HLH kubaini kama kuna makosa yalifanyika au la, lakini pengine si muda wa kuulaumu uongozi wa Hospitali hii ambayo imekuwa ikibeba mzigo mkubwa ambao ulitakiwa ubebwe na serikali hasa kwa kuzingatia kwamba Hospitali hii inahudumia zaidi ya watu milioni mbili.
Ni wakati muafaka kwa wabunge wetu na serikali kwa ujumla kuliweka hili jambo vizuri na kutoa msaada wa mazishi "stahili" kwa marehemu ambao ndugu zao hawana huo uwezo ambao wengi wao hutokea maeneo ya mbali na hapa Haydom.
Vilevile uongozi wa HLH unaombwa kutoa elimu hasa kwa wafiwa wa namna hiyo juu ya utaratibu mzuri wa mazishi na wasiruhusu maiti kutolewa kwa aibu namna hii, pia kuweka utaratibu mzuri ambao ihakikishe unafuatwa kwani matukio kama haya hayailetei picha nzuri jamii yetu na pia kuichafulia jina zuri hospitali yetu. Kama ikiwezekana (sijui kama huwa inafanyika) hawa wafiwa kama hawana uwezo basi wasaidiwe kupata majeneza na usafiri hadi makaburini ili tuheshimu utu wa mwanadamu hata kama ni marehemu, tujue kuwa sisi sote tutakufa na hatujui tutafia wapi na tutazikwaje lakini kila mtu anastahili mazishi ya heshima haijalishi anandugu au la, anauwezo au hana.

Neema ya Mungu na Upendo wa Kristo iwe pamoja nanyi sasa hata milele!

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda