Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Wednesday, June 27, 2012

Hanang wapata mkopo wa matrekta yenye thamani ya zaidi ya sh.mil.370


 Na Mary Margwe,
 Hanang Manyara
Wilaya ya Hanang yaanza kupata matumaini ya utekeleza wa zoezi la mapinduzi ya kilimo kwanza mara baada ya Benki ya Uwekezaji Tanzani (Tanzania Investment Bank  -TIB) kutoa mkopo wa trekta 9 zenye thamani ya zadi ya mil.370.8 kwa wananchama 9 kutoka chama cha kuweka  na kukopa kwa Saccos ya TAKAUMA.

 Akikabidhi trekta hizo jana kwa niaba ya Waziri Mkuu Mstahafu wa awamu ya tatu, Mh,Fredrick Summaye, Mkuu wa Wilaya ya Hanang, Bi.Christina  Mndeme, mbele ya Mbunge wa Viti maalum Mkoanwani Manyara(CHADEMA)  Bi.Rose Kamili, mwenyekiti wa Saccos ya TAKAUMA Bw.Onesmo Kamili, Mkuu huyo alisema shughuli za maendeleo hazina itikadi hivyo sasa ni wakati wa kuchapa kazi tu na si vinginevyo.

Bi.Mndeme alisema trekta hizo 9 zinatakiwa kuleta maendeleo ya haraka ili kuleta  tija katika kuongeza hali ya uzalishaji wa mazao mbalimbali ili wananchi waweze kuongeza  kipato na hatimaye kuondokana na umaskini kupitia  mapinduzi ya kilimo kwanza.

Alisema sasa wakati umefika wananchi wa Jimbo la Hanang kuanza kuona matarajio yao halisi ya mapinduzi ya kilimo kwa kua tayari sasa wameanza kumiliki zana kubwa za kilimo  na hatimaye taratibu baadaye wananchi wote wataanza kuondokana na jembe la mkono,ambao uzalishaji wake haulingani  na dhana kubwa kama trekta.

Aidha alimpongeza Mbunge wa Viti maalum wa Mkoa wa Manayara mhe. Rose Kamili (CHADEMA) kwa kuwa mstari wa mbele katika kufuatilia mkopo huo hadi dakika ya mwisho na kufanikisha zoezi hilo, ambapo aliahidi kushirikiana naye kikamilifu katika kuhakikisha kuwa wananchi wa Hanang wanapata maendeleo ya haraka zaidi kupitia zana hizo za kilimo (trekta) kwa kile alichokidai kuwa ampe ushirikiano  kwani maendeleo hayana itikadi.

“Shughuli za maendeleo zote hazina itikadi hivyo naomba tena nawaomba sana katika shughuli zetu za maendeleo itikadi zetu ziwekwe pembeni  kabisa ili kuweza kusukuma  gurudumu letu la maendeleo ya Wilaya Hanang, kikamilifu ,kwani mara nyingi itikazi mbalimbali huwa zinakwammisha shughuli za maendeleo.

Aidha lisema historia ya Hanang hususani kata ya Basotu  imekua ikijulikana  kama  ni Kijiji  kinachoongoza kwa shughuli za kilimo hususani kilimo cha ngano, mahindi, maharagwe na alizeti  hasa kwa kuzingatia ardhi yao ina ardhi yenye rutuba, hivyo matrekta hayo yatakua chachu ya kulekeleza kauli mbiu ya mapinduzi ya kilimo kwanza katika Wilaya ya Hanang.

“Nimeambiwa na kusikia kuwa kati ya hayo matrekta 9, wanamke aliyejitokeza kukopa ni mmoja tu, huku wananume wakiwa 8,ni nafasi yetu sasa wanawake kuhakikisha tunakua mbele katika kupambana na umaskini kupitia vikundi mbalimbali vya kuweka na kukopa (SACCOS) na si vinginevyo.

Naye Mbunge huyo Rose Kamili  alisema kuwa uhai wa mabadiliko ya kilimo kwanza yanategemea kulima kwa wakati,upatikanaji wa mbegu bora na mbolea iliyo na tija ili kuhakikisha mkulima anajikwamua kiuchumi kupitia kilimo kwanza,hivyo kupatikana kwa matrekta hayo 9 ni matumaini mapya ya kuwakomboa wanachama wa Saccos ya TAKAUMA na wananchi wengine kiujumla.

Mh,Kamili alisema ni dhairi kuwa mapinduzi ya kijani  kamwe hayawezi  kul;etwa na jembe la mkono  bali kwa kilimo kutumia zana bora za kilimo cha kisasa kama vile matrekta  na hivyo kuipongeza bodi ya Tanzania Intestiment Bank (TIB) kwa kua na imani na hiko chama cha kuweka na kukopa cha  Saccos ya MTAKAUMA na hatimaye kupitisha hayo majina 9.

Akizungumzia changamoto mbalimbali hadi kufikia hatua hiyo ya kupatikana kwa dhana hizo za kilimo alisema kuwa ni pamoja na wanachama wa kuweka na kukopa (SACCOS) kuogopa kukopa  kwa madai ya kupoteza fedha zao,na huku wananchi wengi wakiogopa kabisa kujiunga na vyama vya kuweka na kukopa.

Kama nchi yenyewe inadaiwa, mawaziri  na wabunge wote wanakopa, sasa sijui nyie mnaogopa nini kukopa, dawa ya deni ni kulipa na sio kuogopa kulipa hivyo hakikisheni mnakopa na kurejesha fedha hizo kwa wakati”alisema Rose Kamili

Aidha changamoto nyingine kuwepo kwa baadhi ya viongozi  wanaokatisha tama  juhudi za wananchi  kwa urasimu wao bninafsi,kwani wamekua na lugha chafu  za uchochezi  hata kufikia hatua ya kuwaandikia barua wakopeshaji (Benki ya Uwekezaji  Tanzania ) kuwa SACCOS ya TAKAUMA  isipewe mkopo,ambapo hatua hiyo imesababisha idadi kubwa ya wakopaji kupungua tofauti na ilivyokua awali.

Pia alisema gharama kubwa za ufuatiliaji  wa mikopo  imekua ni changamoto kwani wananchi wanalazimika kusafiri zaidi ya kilometa 1000  kwenda Jijini Dar –es- Salaam  kufuatilia mokopo hiyo huku gharama za usafiri zikiwa juu zaidi.

Aidha Bi.Kamili  alitumia nafasi yake katika kuwatahadharisha wanachma hao waliokopa wa Saccos ya TAKAUMA  kutambua kuwa mikopo hiyo inahitaji kurejeshwa  kwa kile alichokidai kuwa ucheleweshaji au ukaidi wa marejesho  utawanyima fursa wananchama wengine  walio na lengo la kukopa,hivyo wametakiwa kuwa waminifu.

Hata hivyo aliwataka wakopaji hao kutowalangua wateja wao (wakulima wengine) watakaotaka kulimiwa mashamba yao kwa kuwapandishia bei ,bali watumie bei za kawaida  na zinazoweza kuwapa unafuu wakulima hao,huku akishauri kwa wakopaji hao kutozitoa  trekta hizo nje ya Wilaya hiyo ya Hanang,kwani kufanya hivyo ni kuhatarisha usalama wa dhana hizo na hivyo kufanya ugumu wa urejeshaji wa mikopo hiyo.

“Ni matumaini yangu kuwa dhana hizi zitatumiwa kwa shughuli za kilimo kadri maelekezo kutoka kwa wataalamu na washauri juu ya kuvitumia ,kuvisimamia, na kuvilinda  ili viweze kufaa  kwa shughuli za kilimo  na kuweza kujikwamua  katika wimbi la umaskini wa kipato  na hatimaye kupiga hatua  kubwa kimaendeleo.

Hata hivyo aliwataka wana SACCOS hao kuhakikisha wanaongeza ushirikiano ,kuwa waadilifu ,na kuchapa kazi kwa nguvu ili kikundi  hiko  siyo tu kiweze kujikwamua kiuchumi bali kwa wananchi  kiujumla  katika Wilaya ya Hanang,kwa kufanya hivyo  Saccos hiyo itakua ni mfano wa kuigwa  miongoni mwa Saccos zingine za Mkoa wa Manyarana hivyo kuwa chachu  ya  kurudisha heshima ya kilimo katika Wilaya hiyo ya Hanang,ambayo kwa miaka mingi imekua ikirudi nyuma.

Naye kwa upande wake Mwenyekiti wa chama cha kuweka na kukopa  Saccos ya TAKAUMA Bw.Onesmo Kamili alisema idadi ya wananchama imeongezeka kutoka 60-kufikia 121 ambapo kati yao wanaume ni 110 huku wanawake wakiwa 11 tangu kilipoanzishwa mwaka 2006.

Bw.Kamili alifafanua kuwa kila mwanachama ana kiasi cha shea y ash.mil.6,150,000 huku akiwa na akiba y ash.mil43,571,000,ambapo alibainisha  kuwa chanzo cha mapato  ni pamoja na ada ya kiingilio,ada ya adhabu,malipo ya kuwa wanachama  na riba inayotozwa kwenye mikopo inayotolewa kwa wanachama.

Akizungumzia changamoto zinazowakabili alisema kuwa licha ya kujitahidi kwa kiasi kikubwa kwa chama kuhamasisha wanawake kujiunga na Saccos lakini  bado mwitikio huo umeshindikana kabisa,ambalo linatokana na  hofu yaokatika kulipa mikopo kutokana na hali nguvu  ya uchumi  waliyonayo wanawake,na hivyo bado inawasisitiza kujiunga ili kuweza kujikomboa kiuchumi na kupunguza umaskini kama si kumaliza kabisa.

Hata hivyo alimpongeza Mbunge huyo wa viti maalumu Bi.Rose Kamili kwa kuwaunganisha  na Tanzania Investiment Bank (TIB),na Chma cha wakulima Tanzania kwa kuuwaunganisha katika mikopo ,kumwezesha mwenyekiti huyo pamoja na timu yake katika kufuatilia makampuni mbalimbali  kwa ajili ya kupata mikopo,kadhalika kuwapeleka katika wasambazaji mbalimbali bila kuchoka kwa kutafuta unafuu  wa bei na ubora wa trekta ambapo walifanikiwa kumpata Mkurugenzi wa kampuni ya
Kihelya Auto Tractor Parts Ltd, Bw.Lazaro Kihelya

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda