Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Thursday, June 28, 2012

Halmashauri (W) Mbulu yawafukuza kazi wafanyakazi 18Na Mary Margwe,
Mbulu Manyara

Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara  imewasimamisha kazi watumishi 18 kutoka idara mbalimbali kuhusiana na  tuhuma mbalimbali za uvunjaji  wa kanuni za maadili ya utumishi wa umma.

Hayo yalibainishwa jana na Mwenyekiti wa Kamati ya fedha Uongozi na Mipango, Bw.Joseph Mandoo, wakati alipokua akiwakilisha taarifa hiyo kwenye kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashari hiyo.

Bw.Mandoo ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, alisema watumishi hao wamekua wakionywa mara kwa mara kuhusiana na uvunjaji wa kanuni za maadili ya utumishi wa umma, lakini bado wamekua wakigaidi na hivyo Halmashauri kuchukua hatua kama hiyo.

Aidha Bw.Mandoo alisema kati ya hao watumishi 18 waliosimamishwa kazi, watumishi 12 ni walimu huku 6 wakiwa ni maafisa watendaji wa vijiji (VEO), ambao mashauri yao yanaendelea kushughulikiwa katika vyombo mbalimbali vya masuala ya nidhamu  na vyombo vya kisheria.

Akifafanua alisema  maafisa watendaji hao 6 wamesimamishwa kazi kutokana na tuhuma ya kushindwa kuwasomea wananchi taarifa ya mapato na matumizi katika Vijiji, huku watumishi 12 ambao ni walimu wakihusishwa na kusa ama tuhuma ya utoro kazini, jambo lililopelekea Halmashauri kuchukua hatua za kinidhamu.

Aliwataja maafisa watendaji na vijiji kwenye mabano kuwa ni pamoja na Bw.Dohho Humbaay (Kijiji cha Guwang), Bw.Marco Bura Sanka(Dirim) Bw.Markiadi Tlehhema Zakaria(Ng’wandakw) Bw.Severine Angress(Moringa) Bw.Blasi S.Guli (Gunyoda) na Bw.Nawe Kwaangw(Mangisa).

Kwa upande wa walimua aliwataja kuwa ni pamoja na mwalimu J .Waitara, J.Christopher, J.Hayduwe, S.Shauri, T.John, D.Safari, Y.Augustino,Silas Duway, Said Abdallah , G.Sulle ,B.Chilewa, na Bw.D.Mathayo,ambao wote kwa pamoja  mashauri yao yako kwa Katibu wa idara ya nidhamu (TSD) Wilaya.

Akiongea na "Ohayoda" jana,  mwalimu Bezarel Chilewa alisema yeye shauri lake haliko kwa katibu wa wa idara ya nidhamu (TSD) Wilaya kama ilivyotamkwa hapo juu, bali liko mahakama ya Mkoa wa  Mnayara Mjini Babati kwa takribani yapata  miaka mitano (5) sasa.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda