Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Thursday, June 21, 2012

Erasto Mbwilo: Mapadri, Wachungaji na Mashehe wahamasisheni waumini wenu kuhusu sensaNa Mary Margwe,
Mbulu Manyara

Mkuu wa Mkoa wa Manyara Bw.Elaston Mbwilo ametoa rai kwa viongozi wa dini hasa Mapadri, Wachungaji pamoja na Mashee kuhakikisha kuwa wanazungumzia umuhimu wa sensa kwa wananchi mara wanapokua makamanisani na misikitini kwani wao kwa kuwa wanauwezo mkubwa wa kutoa elimu hiyo.

Akiongea katika kikao cha wadau wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, kilichofanyika jana katika ukumbi wa maendeleo ya jamii Wilayani hapo, Bw.Mbwilo alisema Mapadri, Wachungaji na Mashee kuwa wananafasi kuwa ya kuongea na waumini wao kuliko hata viongozi wa Chama na Seikali kwani wanakutana nao  mara kwa mara.

Alisema sensa itaisaidia Serikali kuweza kupanga mipango yake ya kutoa huduma kwa wananchi wake kikamilifu, kwa umakini kwani bila hivyo Serikali itashindwa kupanga mipango yake ya maendeleo kwa wananchi wake kulingana na idadi ya watu wake na makazi.

“Mwaka huu ni mwaka wa sensa ya watu na makazi  nchini itakayofanyika Agosti 26 mwaka huu, ambapo alisema ni  miaka 10  baada ya sensa  ya mwisho iliyofayika  mwaka 2002 hivyo tunatakiwa kuhakikisha kuwa kila mmoja kwa nafasi yake aliyonayo katika jamii anatakiwa kuzungumzia suala la sensa”

Aidha alisema kuwa hatapenda kusikia kuwa Mkoa wake umeshindwa kutekeleza suala hilo la sensa kwa kile alichokidai kuwa kinyume na hivyo wananchi wa Mkoa huo hawatafanikiwa kupata fedha za miradi mbalimbali ya maendeleo, hivyo wametakiwa kuhakikisha suala hilo linatekelezwa kwa asilimia mia moja (100%)

Naye Mratibu wa Sensa Wilaya  Bi.Mary Kabigi alisema mwaka  huu sensa hiyo itakua ni ya tano kufanyika tangu  Tanzania kupata uhuru, ambapo zilizopita zilifanyika katika miaka ya 1967, 1978,188 na 2002.

Bi.Kabigi alifafanua kuwa, ili kupata ushirikiano mzuri  na wenye ufanisi  kutoka kwa watu  wote, ni muhimu kufanya jitihada za uhamasishaji  unaolenga  kuelimisha jamii ili kufahamu umuhimu wa zoezi hilo la sensa na si vinginevyo.

Akizungumzi lengo kuu la uhamasishaji ni kuhakikisha kuwa wananchi wote wanaelewa umuhimu wa sensa ili waweze kutoa ushirikiano na kushiriki  kikamilifu katika zoezi zima la sensa.

“Maana ya sensa ya watu na makazi ni zoezi maalum lenye lengo la  kupata idadi ya watu  wote  katika nchi, kwa umri, hali yao ya elimu, kwa umri na jinsia, mahali  ya ajira, hali ya vizazi na vifo na hali ya makazi ama ni  utaratibu wa kukusanya, kuchambua, kutathimini na kuchapisha au kusambaza  takwimu  za kidemografia, kiuchumi na kijamii kuhusiana na watu wote  na makazi yao katika nchi  kwa kipindi maalum" Alisema Bi.Kabigi

Hata hivyo alisema sensa ya watu na makazi  hufanyika katika katika nchi zote ulimwenguni, zilizoendelea huendeshwa kwa kufuata kanuni, taratibu  na miongozo maalum  iliyokubalika kimataifa, ni utaratibu unaofuatwa na nchi nyingi  Tanzania ikiwa ni mojawapo, ambapo hufanywa kila baada ya miaka 10.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda