Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Thursday, June 14, 2012

Endagew wapokea PETS kwa mikono miwili

Baada ya semina ya siku tatu iliyokuwa inatolewa na Kituo cha utamaduni cha Haydom (4CCP) kwa kushirikiana na Norwegian Church Aid iliyolenga kutoa mafunzo ya ufuatiliaji wa mapato na matumizi ya fedha za umma (Public Expenditures Tracking System-PETS) kwa wenyeviti na maafisa watendaji wa vijiji na wanasheria wasaidizi (paralegals) kutoka wilaya tatu za Iramba, Hanang na Mbulu, zoezi la kuhamasisha uundaji wa kamati za PETS vijijini lilianza rasmi leo ambako timu ya 4CCP na ile ya NCA walienda katika kijiji cha Endagew kata ya Getarer kilichopo wilaya ya Mbulu walipewa elimu kuhusu PETS.
Wanakijiji hao walilipokea kwa mikono miwili wakisema kuwa PETS ni jambo zuri sana japo limechelewa kuanza kwani kama ingekwepo mapema ubadhirifu mkubwa wa fedha za umma ungeweza kudhibitiwa.
Endagew na Endaharghadatk ni vijiji viwili vilivyoteuliwa kuwa vijiji vya mfano (pilots) katika utekelezaji wa PETS na baadaye vijiji vingine zaidi vitahusishwa.
Akizungumza na Ohayoda mwakilishi wa NCA, Gilbert Mworia alisema kuwa vijiji hivi viwili vitatumika kutoa tathmini kama zoezi hili litakuwa endelevu au la na kuongeza kuwa madhumuni ya shirika lao ni kuwawezesha wananchi kuweza kuuunda kamati zao wenyewe na kufuatilia matumizi ya fedha za serikali kuanzia ngazi za chini kabisa
 Timu ya 4CCP na NCA ikiwasili Endagew
 Mbele ya wananchi
 Afisa mtendaji wa kijiji cha Endagew ndugu Herson akitoa utambulisho


Mkutano ulipoisha

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda