Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Friday, June 1, 2012

CWT Mbulu yatoa semina kwa walimu wakuu  • Yalenga kuinua taaluma hasa katika somo la English, Hisabati na Sayansi
  • Yatoa vitabu 540 kwa shule zote 135 za wilaya ya Mbulu


Na Costas Onna-Mbulu
Chama cha Walimu Tanzania (CWT) wilaya ya Mbulu kikishirikiana na shirika moja lisilokuwa la kiserikali kutoka Uswisi la HELVETAS limefanya seminar kwa walimu wakuu kutoka shule 28 za msingi katika wilaya ya Mbulu yenye lengo la kuimarisha somo la Kiingereza (English) na Mazingira (Environmental studies) mashuleni.
Semina hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa kituo cha walimu Endagikot-Mbulu ilifunguliwa na mwenyekiti wa CWT wilaya ya Mbulu ndugu Wensenslaus L.Musenya ambaye aliwataka walimu hao kutumia elimu watakayoipata kupitia semina hiyo kwa ajili ya kuboresha taaluma katika shule zao.
Aidha katibu wa CWT wilaya ya Mbulu ndugu Zacharia B. Naali akizungumza na Ohayoda alisema kuwa semina hii ililenga kutoa mafunzo kwa wakuu wa shule 28 wa shule mpya na zilizopo pembezoni ambao hawakupata mafunzo katika awamu za awali za mradi huo wa mafunzo.
Alizidi kueleza kuwa uchunguzi umebaini kuwa kiwango cha ufaulu hasa katika somo la English kimekuwa duni sana toka 2004 na pia CWT imedhamiria kuwawezesha walimu kuboresha mazingira ya kufundishia ili yawe kichocheo kwa wanafunzi kujifunza hasa katika kuweka usafi
``Hizi ni shule 28 za mwisho kati ya 135 katika wilaya yetu kupata haya mafunzo, baada ya mafunzo haya tunatarajia kufanya pia mafunzo ya siku 5 kwa ajili ya walimu wa English kutoka shule hizi 28 ambao bado hawajapata mafunzo`` alisema Ndugu Naali
Naali alizidi kueleza kuwa CWT wilaya ya Mbulu imedhamiria kuongeza wigo wake wa utendaji zaidi ya kutetea maslahi ya wanachama wake yaani walimu ambao hukatwa 2% ya mshahara wao kuchangia shughuli za Chama hicho na kuboresha taaluma ya wanachama wake kupitia mafunzo mbalimbali.
"Baada ya awamu hii kukamilika, tutafanya mafunzo kwa ajili ya walimu wa Hisabati na Sayansi ili kuongeza hamasa na kuinua kiwango cha ufaulu katika haya masomo yanayokimbiwa na wengi na kuanzia watachagua mwalimu mmoja kwenda kwenye mafunzo yatakayoandaliwa na CWT Mkoa wa Manyara.
"Tutamchagua mwalimu mahiri katika somo la hesabu na sayansi kwa ajili ya kupata mafunzo ambaye atachaguliwa na wanachama wenyewe na pia kupitia kwa wakaguzi na kupitia vituo vya walimu"
Naali aliwasihi walimu waliopata mafunzo hayo kuyatumia kuboresha taaluma katika vituo vyao vya kazi ili iwe na manufaa kwa Taifa na kuongeza viwango vya ufaulu. CWT tunajitahidi kuwasaidia wanachama wetu kufanya kazi katika mazingira bora zaidi na pia imekwishatoa vitabu 4 (ikiwemo dictionary 1) kwa kila shule na mpaka sasa imetoa jumla ya vitabu 540 kwa shule zote.
Naye Daniel Shango ambaye alishiriki semina hiyo alisema hii ni mara yake ya pili kushiriki semina hii na kusifia jitihada zinazofanywa na CWT katika kuboresha taaluma
 "nimefurahishwa sana jinsi Chama cha Walimu kinavyosaidia kutoa semina kama hizi na katika semina hii washiriki huelezwa namna ya kuboresha taaluma pia washiriki hupewa vitabu vya kiada na safari hii vitabu walivyopewa washiriki hii hivi hapa"

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda