Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Tuesday, June 19, 2012

Bung`eda: Kilele cha mazishi ya kidatoga katika Picha

Siku ya Jumamosi ya Tarehe 16 June 2012 ilikuwa kilele cha Mazishi ya mzee wa kidatoga aliyekuwa anaitwa Gidmarirda na hivyo katika harakati zetu za kuandaa filamu kuhusu Historia, Maisha na Hatma ya Wadatoga tulipata fursa ya kupiga picha matukio halisa katika tukio hilo yaani "Bung`eda Gidmarirda (Bung`eda ya Gidmarirda). Haya ndiyo yaliyojiri....
Hapa ni semosii (CMSC) yaani Central Maintenance and Servicing Center ya iliyokuwa Shirika la Chakula la Taifa (NAFCO). Njia panda ya kulekea Nyabat

Biashara nazo zilichukua mkondo wake.....Mama Happy akibagain bei

Watu walitoka sehemu mbalimbali, biashara mbalimbali hasa ya vyakula ilibamba sana

Kama kawa kama dawa, nachukua matukio live bila kuigiza wala kuigizwa

Watu wakiwa wamezunguka Bung`eda huku wakicheza ngoma

Bung`eda upande wa kushoto, hilo ndilo kaburi alimozikwa mtu akiwa kakaa

Hiii inaitwa "Gidgeta" yaani kipimio cha asali kwa ajili ya kutengeneza pombe ya Gesuda


vitendea kazi, gidgeta kwa ajili ya kupimia asali, kibuyu cha pombe na pembe kwa ajili ya kuwaonjesha wengine


Hizi ndizo Gesuda, kila kibuyu kina ujazo wa takribani lita 30 na hapa ndipo pombe ya gesuda inapoandaliwa kwenye nyumba maalum vikiwa vimepangwa zaidi ya vibuyu 30

Tulipata upendeleo wa kuruhusiwa kuchukua picha kwenye "brewery" hii ya ukweliHizi ni nyumba zilizojengwa kwa ajili ya wageni, zipo zaidi ya 50 na kila moja inachukua wanafamilia zaidi ya 20


Hapo vipi? Wakiwa wanatembea ni zaidi ya Mamodo

Niliwakuta hawa jamaa wakiwa"protect" dada zao ili wasitekwe na kuolewa kwa nguvu, yaani ukikuta mwanaume na msichana ambaye hajaolewa pamoja ujue ni kaka yake anamlinda asiibiwe

Pembeni ya eneo la tukio kuna "Basonyabat" yaani ziwa nyabat, nilipelekwa hapo na hawa machalii wangu wa ukweli

Kila mtu na rangi yake ya "mgorori" hakuna kuiga 

Ori wa ukweli sana hawa

Kila kona watu kibaoHakuna kabila Tanzania linalopiga maurembo ya kweli kama hawa jamaa, hawa ni mabinti "uda" ilibidi niuze nao sura 

"Hata sisi tunaweza kupozi kwa ajili ya picha ati"

"Do you see me?" pete za ukweli, shingoni, mikononi miguuni dah usipime

Ngoma zikashika hatamu sehemu nyingine

Warembo wakiwa kwenye ngoma


Hawa ni vijana mashujaa walioamka alfajiri saa 10 kwenda kuchukua "lelechand" katika ziwa Balang`dalalu zaidi ya 40Km kutoka hapo wakirejea saa 12 jioni kwa shamrashamra

Hii ndo lelechanda, haya majani yanawakilisha nywele za marehemu na huwekwa juu ya Bung`eda katika kuhitisha shughuli

Nikajitosa kati bila hofu wala wasiwasiHii ni ngoma ya kina mama wa "rika" la marehemu

Wairaqw nao wakaona isiwe tabu nao wakashusha ngoma yao pembeni kidogo, burudani ilikuwa si ya kitoto

Kama Anderson Cooper wa CNN vile

Huyu dogo alikuwa habanduki kila ninapokuwa 

Watu walikuwa kibao kila sehemu, hadi juu ya miti

Camera yetu ilimnasa huyu chalii akiuza "viroba" katika eneo la tukio


Baada ya tukio hilo, watu wote walitawanyika baada ya wengi kukaa hapo kwa takribani mwezi mzima, na nyumba hiyo nayo ikawa hame.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda