Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Friday, June 8, 2012

"Bomoa Bomoa" Mbulu: Vibanda vya stendi vyabomolewa

  •  Zoezi hilo kuendelea hadi Haydom na Dongobesh

  • Vurugu zatokea, Polisi waingilia kati

  • Waliojenga bila vibali nao kukumbwa na "bomoa bomoa " hiyo

  • Waliojenga kabla ya upimaji wanatakiwa kuwasilisha ramani za nyumba zao 

  • Waliojenga bila kufuata ramani za majengo waliyowasilisha wakati wanaomba vibali nao hatarini

 

Vibanda vilivyobomolewa (Picha na Costas Onna, Mbulu)

Na Mwandishi wetu

Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu kupitia Idara ya Ardhi jana iliendesha zoezi la kubomoa vibanda vilivyojengwa kiholela bila kufuata utaratibu katika Stendi ya Magari ya Mbulu. Akiongea na Ohayoda kwa njia ya simu, Afisa Ardhi wa Wilaya ya Mbulu ndugu Deogratius Mathiya alisema zoezi hilo litaendelea katika mji mzima wa Mbulu na kisha litahamia Haydom.
"Leo (jana) tumebomoa jumla ya vibanda 10 vilivyojengwa bila kufuata ramani ya eneo la stendi, lakini zoezi hili halitaishia hapa tutaendelea kusafisha sehemu zote za mji wa Mbulu vikiwemo sokoni na barabara za vichochoroni ambazo watu wamejenga kiholela" Alisema Mathiya
Ohayoda ilitaka kujua kama zoezi hilo litaishia Mbulu tu au litaendelea sehemu zingine afisa huyo mwenye dhamana ya kuongoza idara hiyo nyeti alisema;
Stendi safiiii
"Zoezi hili halitaishia Mbulu tu, tukimaliza Mbulu tutahamia Haydom na Dongobesh kusafisha maeneo yote ambayo watu wamejenga kiholela bila kufuata utaratibu ikiwemo stendi na waliojenga katika hifadhi za barabara za ndani ya mji, tunawasihi wananchi hasa waliojenga kinyume na taratibu wazingatie sheria ili wasipate hasara"
"Tutabomoa nyuma zote zilizojenga kiholela katika viwanja vidogo vya stendi za Mbulu na Haydom na tutapita Mbulu, Haydom na Dongobesh katika viwanja vyote kulingana na ramani ya mpango mji na kama kuna mtu amejenga kinyume na ramani ya mpango mji nyumba hizo zitabomolewa"
Mathiya alizidi kueleza kuwa watakagua vibali vya ujenzi ikiwa ni pamoja na ramani za nyumba zilizowasilishwa wakati wa kuomba vibali hivyo ili kubaini kama ujenzi umefanyika kulingana na vibali vilivyotolewa kwa mujibu wa sheria na kama ujenzi umefanyika kinyume na vibali hivyo au ramani tofauti na ramani iliyowasilishwa idarani kwake nyumba hizo nazo zitabomolewa au wahusika wazirekebishe ziendane na ramani iliyowasilishwa.
"Hata waliojenga ndani ya ramani ya mpango mji lakini tofauti na ramani waliyowasilisha wakati wanaomba vibali vya ujenzi nyumba hizo zitabomolewa au wazirekebishe ziendane na ramani waliyowasilisha. Kwa waliojenga kabla ya upimaji (mpango mji) wanatakiwa wafike katika ofisi za ardhi ili wapatiwe vibali lakini kwa waliojenga baada ya zoezi la upimaji pasipo kupata vibali rasmi watawajibika kisheria kwani wanapaswa kufuata sheria na taratibu zinavyotaka" alisema Deogratius Mathiya
Aidha katika hatua nyingine zoezi hilo liliingia doa baada ya kutokea vurugu wakati wa kuendesha zoezi hilo lakini hali ya utulivu ilirejea baada ya polisi kufika na kuwatuliza wananchi hao ambao walikuwa wanapinga zoezi hilo kufanyika wakidai kuwa halikufanyika kihalali na hatima zoezi hilo kukamilishwa jana kwa "kusafisha" eneo hilo la stendi ambako vibanda 10 vilikumbwa na dhahama ya kubomolewa.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda