Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Friday, June 15, 2012

AFYA KWANZA MAMBO YA KUFANYA UNAPOUUNGUA SEHEMU NDOGO


Na Beatrice Githiri-HLH
 Habari za leo wapenzi wasomaji wa Ohayoda hasa wa makala hii maridhawa ya AFYA KWANZA ambayo inalenga kutuwezesha kuwa na afya bora kwa ustawi wetu. Leo tutaangalia mambo ya kufanya unapoungua moto sehemu ndogo ya mwili wako.
Mara nyingi katika kazi za ndani au nje ya nyumbani tunaweza kuungua kwa bahati mbaya. Mifano ya vitu vinavyoweza kutusababishia kuungua ni maji ya moto, chai, moto wenyewe, sufuria na n.k. kama umeungua sehemu ndogo mara nyingi tunaweza kujihudumia na kuepusha madhara zaidi.

  1. Pooza sehemu iliouungua
Weka sehemu iliouungua kwenye maji yanayotiririka bombani kwa dakika 15-20, au dumbukiza kwenye maji ya baridi au weka cold compress kwa mda wa dakika 15-20.

  1. Usiwekebarafu moja kwa moja katika sehemu ilouungua
 Kuweka barafu kwenye sehemu iliouungua kutafanya uungue na baridi zaidi na kukusababishia madhara zaidi.

  1. Funika sehemu iliouungua
Funika sehemu iliouungua kwa kutumia gauze ambayo imetakasika(sterile). usibane  au kukandamiza ili kuepusha msukumo (pressure). Kufunga husaidia kuzuia hewa isipita na kupunguza maumivu.

  1. Usipasue lengelenge
 Sio vizuri kupasua lengelenge ambalo utapata baada ya kuungua. Kama maumivu yatakuwa makali sana toboa sehemu ndogo sana na kitu ambacho kimetakasika na kisha usafishe na sabuni ya antibacterial au maji ya chumvi.

  1. Pata dawa ya maumivu na paka lotion
Dawa za aumivu kama aracetamol, asprin na brufen zinasaidia kupunguza maumivu.
Pia kama utapata lotion za kusaidia kuungua ni vizuri kupaka mara baada ya kupooza sehemu iliouungua.
Epuka kupakaa mafuta sehemu iliouungua.

Wapenzi wasomaji wetu, tunakaribisha maoni, maswali na ushauri kuhusu makala hii au pia kupendekeza mada (topics) zipi ziweze kuwasilishwa kwenu wasomaji nasi tutalifanyia kazi.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda