Wasomaji wa Ohayooda, nawashukuru kwa
kuendelea kusoma makala ya afya ambayo inaendelea kuwaelimisha jinsi yakufanya
maishha yako yawe ya afya zaidi.
Usingizi
ni sehemu ya mapumziko kwetu kutokana na
kazi za mchana ambazo zinatuchosha. Wengine wanasema usingizi ni afya. Je
unapata usingizi mzuri na wakutosha?
Kutopata
usingizi mzuri na wakutosha kunaweza kusababisha usahaulifu na matatizo ya
kuweza kuwa makini (concentration).
Yafuatayo
nimambo ya kufanya ili kukusaidia kupata usingizi unaofaa.
- Punguza muda wako kitandani
Kukaa
au kujilaza kitandani muda ambao sio usiku kutakufanya ukose usingizi mzuri wakati wa usiku. Epuka kuwa kitandani muda mrefu.
- Usilazimishe usingizi
Soma au
angalia Tv hadi usinzie ndipo uende chumbani kulala. Lala na amka muda sawa
kila siku ili kuzoeesha mwili wako muda wa kulala na kuamka.
- Ficha saa ukiwa unakosa usingizi
Kuangalia
saa ili kuona umekosa usingizi kwa mda gani kutakupa wasiwasi zaidi na
kuendelea kukufanya ukose usingizi.
- Epuka au punguza caffeine, uvutaji sigara au ugoro na pombe
Caffeine
ni kichangamshaji (stimulant). Nicotine iliokokwenye sigara pia huadhiri
usingizi. Pombe ni depressant – hufanya mwili kulegea na inaweza ukufanya
kusinzia lakini ni kwa muda mfupi tu na badae kukunyima usingizi.
- Fanya mazoezi
Kufanya
mazoezi au zoezi lingine linalohusisha misuli
kutakusaidia kupata usingizi mzuri. Jitahidi angalau nusu saa walau siku
3 za wiki au zaidi kwa wiki.
Usifanye
mazoezi karibu na muda wa kulala ili usiingilie usingizi wako.
- Kuwa
mwangalifu na unachokula kabla ya kulala
kula
chakula laini kabla ya muda wa kulala. Epuka chakula kizito, pia baada ya mlo
wa jioni.
Epuka
kunywa vinywaji vingi kabla ya muda wa kulala ili usiamke mara nyingi kwenda
haja ndogo usiku.
- Epuka kusinzia mchana
kusinzia
mchana kutakufanya ukose usingizi usiku. Endapo unalazimika kulala, usizidishe
nusu saa ili kuepuka kuingilia usingizi wako wa usiku.
- Pata ushauri kuhusu dawa unazotumia
Kama
kuna dawa zozote unazozitumia ni vizuri upate ushauri kutoka kwa daktari ili
kujua kama zinaweza kuathiri usingizi wako.
Dawa ziwe za hospitali au za kununua katika duka la dawa ni vyema kuelewa kama mfumo wake wa kufanya kazi mwilini unaweza kuadhiri
usingizi wako usiku.
No comments:
Post a Comment