Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Friday, June 8, 2012

AFYA KWANZA: JINSI YA KUTIBU DONDA KOO ISIYO KALI (MINOR SORE THROAT PAIN)Na Beatrice Githiri-HLH
 Mara nyingi hili tatizo linatupata na tunadhani ni mafua japo inaweza kuwa shida nyingine. Tunaweza kutibu au kupunguza dalili zake kwa kufuata maelekezo nitakayoyatoa. Endapo utapata dalili zifuatazo au ukiwa na hili tatizo ni muhimu umwone daktari mara moja. 
  • Homa
  • Kichefuchefu
  • Kutapika
  • Tezi za shingo kuvimba
  • Kushindwa kuhema au kumeza
  • Tezi zenye usaa ( tonsils with pus)
  • Maumivu makala ambayo hayapungui

Jinsi ya kupunguza maumivu

1.      kunywa vitu vingi vya majimaji

Kuwa na maji mwilini ya kutosha kunasaidia kulainisha makamasi hivyo kuwa rahisi kutoa kikohozi au makamasi.

2.      sukutua kwa maji ya vuguvugu ya chumvi

Changanya kijiko kidogo cha chumvi na maji ya vuguvugu glas1 moja  kisha sukutua, hii inasaidia kupunguza makamasi au kikohozi kwenye koo.

3.      mumunya pipi kali au tafuna bubblish isiyo na sukari

Kumumunya hivi vitu kunasaidia mate mengi kutoka au kutengenezwa hivyo kusafisha koo lako

4.      Jaribu dawa za maumivu

Nunua dawa za kupunguza maumivu kwa mfano brufen au paracetamol au nyingine.

5.      Pumzisha sauti yako

Ikiwa donda koo linahusisha njia ya hewa ,epuka kuongea sana kwa sababu itazidisha muwasho na waweza kupoteza sauti kwa mda.

6.      Hakikisha hewa sio kavu

Hakikisha hewa sio kavu ili kupunguza muwasho.

7.      epuka hali ya hewa chafu

Epuka uvutaji wa sigara au kukaa kwenye chumba chenye moshi au sehemu yenye harufu kali.

 Kama maumivu yataendelea nenda Hospitalini au kituo cha afya kilichokaribu

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda