Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Wednesday, June 27, 2012

ABIRIA ALAZIMISHWA KUKAA NA MAITI KWENYE KENYA AIRWAYS

Na Seth Katende
Africa kuna mambo sana aisee. Hii imetokea juzi tu hapa, Mwanamke mmoja raia wa Sweden alikuwa akisafiri kuja Tanzania kwenye Likizo yake kwa ndege ya KENYA AIRWAYSAkielezea tukio hilo,mwanamke huyo anasema jamaa huyo aliyekaa nae alipandia ndege kwenye uwanja wa ndege wa Amsterdam.

Mshkaji alikuwa anaumwa na alionekana akitokwa na jasho jingi sana na kuchechemea, lakini alilazimisha kusafiri.

Muda mfupi tu baada ya Safari kuanza yule abiria alionekana kuzidiwa zaidi na wahudumu walijitahidi kuwa karibu nae muda wote lakini Izraili alionyesha Umafia wake wa ku-operate hadi angani, yule jamaa aliaga dunia wakiwa katikati ya Safari.

Mwanamke yule kuona vile ikabidi aombe kubadilishiwa Siti lakini kwa Mshangao akajibiwa kuwa ndege imejaa na hakuna popote wanaweza kumpeleka zaidi ya yeye kukaa palepale na ile maiti.

Masaa karibu 10 yule mwanamke alisafiri akiwa amepozi na ile maiti just next seat.

Mawanamke huyo, Lena Petterson alipofika Dar es Salaam aliuandikia uongozi wa Kenya Airways kulalamikia ishu hiyo na ndipo Uongozi ulipoamua kumrudishia Nusu ya Nauli yake kama part ya kumpoza moyo Mwanamama huyo.

Nauli aliyolipa Mwanamama Lena Petterson ilikuwa Dola 1400 na alirudishiwa Dola 700 kama Compensation kwa yeye kukalisha siti moja na Maiti na Mwanamama huyo alikubali Fidia hiyo na kuwa mpole.

Sasa kama hiyo ni Kenya Airways ambao wako very smart kwenye operation zao, Usishangae Air Tanzania ukiambiwa ukae na Magunia ya Viazi uyapakate tena kwenye Siti sitashangaa!


Sourec: http://www.sethought.blogspot.com/

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda