Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Monday, June 25, 2012

45 Wakamatwa kwa makosa mbalimbali Manyara

Na Mary Margwe,Babati
Katika harakati ya kupambana na uhalifu Jeshi la Polisi Mkoa wa Manyara, limefanikiwa kukamata watuhumiwa 45 wakihusika na makosa mbalimbali  ikiwa ni pamoja na utumiaji wa bangi , mirungi,gongo, katika msako na kuimarisha doria  katika maeneo mbalimbali  ya Mkoa huo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana ofisini kwake, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Manyara, ACP. Akili  K. Mpwapwa alisema msako huo ulifanyika kati ya mwezi Juni 9-23 mwaka huu ambapo jumla ya watuhumiwa wapatao 45 walikamatwa wakihusishwa na makosa mbalimbali.

Kamanda Mpwapwa alisema kuwa msako huo una lengo la kuhakikisha kuwa Mkoa huo unakua shwari  na si vinginevyo ili kuhakikisha kuwa wananchi wanakua na amani  usalama  katika utendaji wao  wa kazi za kujiletea kipato.

Aidha alifafanua kuwa kufuatia msako huo Jeshi la Polisi  lilifanikiwa kukamata watuhumiwa 8 wakiwa na kiasi cha misokoto 2,447  ya bangi ikiwa ni sawa na kg.15, watuhumiwa 10 walikamatwa wakiwa na kilo 83.5 za mirungi.

Alisema watuhumiwa 16 walikamatwa wakiwa na lita 105 za pombe haramu ya gongo huku watuhumiwa 11 walikamatwa wakiwa na  kiasi cha kilo 1000 za samaki waliovuliwa bila kibali katika ziwa burunge, ambao waliuzwa  kwa njia ya mnada mara baada ya kupata kibali toka mahakamani.

“Tulifanikiwa kukamata kiasi cha samaki  kilo 1000 waliovuliwa kinyume na taratibu, samaki hao walivuliwa bila kibali, ambao  waliuzwa kwa njia ya mnada mara baada ya kupata kibali cha mahakamani na tayari watuhumuwa wote 11 wameshafikishwa mahakamani” alisema Kamanda Mpwapwa.

Akizungumzia kwa upande wa makosa ya usalama  barabarani, Kamanda Mpwapwa alisema jumla makosa 232 ya usalama barabarani yalikamatwa  ambapo kati yake makosa 119 wahusika walilipa faini na kuwezesha kupatikana jumla ya sh. Mil 5.880,000/=.

Aidha alisema kufanikiwa kwa kiasi kikubwa kufuatia kuwepo kwa  Mahusiano mazuri baina ya Jeshi la Polisi na raia wema ambao kwa namna moja au nyingine walitoa taarifa zilizowezesha zoezi hilo kufaniki kwa kiasi hicho.

“Operesheni hii imefanikiwa  kwa sababu ya kuwepo kwa mahusiano mazuri baina ya Jeshi la Polisi na raia wema  kwa namna moja au nyingine walitupatia taarifa zilizowezesha zoezi hili kufanikiwa kwa kiasi hiki”alisisitiza Kamanda huyo.

Aidha kufuatia hilo alitoa wito kwa wananchi Mkoani hapo kuondoa wasiwasi  na hatimaye kuweza kutoa taarifa mbalimbali zitakazowezesha kufanikisha matarajio ya Jeshi hilo ambayo ni “ kuzuia /kupunguza uhalifu katika Mkoa wetu”

Hata hivyo Kamanda Mpwapwa alitoa rai kwa wananchi wote wanaojihusisha  na vitendo vya uhalifu kuhakikisha wanaacha mara moja kwani Jeshi hilo limejipanga kikamilifu  katika kupambana  na uhalifu  wa aina yoyote ile,huku akidai kuwa kwa wale ambao wataendelea  kujihusisha  navyo hawatasita kuwachukulia hatua kali za kisheria.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda