Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Monday, May 14, 2012

Zijue Taratibu za Kufuata unapotaka Kuoa MWIRAQW

Mu hali gani wapenzi wasomaji wa Ohayoda, karibuni tena katika makala nyingine ambayo leo inahusu taratibu za kufuata kama unataka kuoa katika jamii ya Wairaqw. Kabla ya kuendelea na makala hii napenda kutoa shukrani za dhati kwa Arthur Albinus Awet kwa kuomba Ohayoda ichunguze na kisha kuwafahamisha wasomaji wake kuhusu hizo taratibu kwani vijana wengi  wa ``siku hizi`` hawazijui.
Aidha Ohayoda inapenda kutoa shukrani za pekee kwa Mzee Modesti Gilyo kwa kukubalu kuongea nasi na kutueleza kinagaubaga taratibu zinazohusika.....twende kazi...

Hatua ya Awali: Kuchunguza kama ni ``Housewife Material``


 • Je unampenda?
 • Tabia zake zipoje? nidhamu, uchapakazi na utaratibu ni mambo ya kuzingatia
 • Familia yake ipoje? wanahistoria ya uuaji, sifa mbaya, ukorofi, uchawi au magonjwa ya kurithi?
 • Ni mcha Mungu? (Hata dini ya jadi)
 • Je ni mlevi wa pombe au sigara?
 • Ukarimu ni jambo la muhimu, asiwe mchoyo
 • Utulivu, yaani si mtembezi (anaweza kudumu na familia)
Ili kuweza kujiridhisha inakubidi kufanya uchunguzi wa muda usiopungua miezi sita (miezi 6) kama msichana huyo yupo kwenye mazingira uliyopo na kama anaishi mbali na hapo (hamuonani mara kwa mara) uchunguzi huchukua zaidi ya mwaka moja.

Hatua ya pili: ``Kutangaza nia``

Baada ya kujiridhisha katika hatua ya awali na ukishaona kuwa anakufaa, unaenda kutangaza nia kwa msichana, kama ``saundi`` zako zikaeleweka unamwomba ridhaa ya kuwataarifu wazazi, wa kwako kwanza na kisha wa kwake, naye ataenda kumjulisha mama. Wazazi wako watapenda kujua hasa yale mambo ya hatua ya awali na kama waki``approve`` watataka kujua kama kuna ujamaa. Hauruhusiwi kuoa endapo
``mmetoka ukoo moja, ukoo wa mama yako, ukoo wa bibi mzaa baba na ukoo wa bibi mzaa mama, ukoo wa mama mzaa bibi upande wa mama na ukoo wa mama mzaa bibi upande wa baba``
Kama anaqualify, taratibu za ushenga zinaanza, mshenga anaweza kuwa baba mzazi au mzee yeyote ambaye ni mwaminifu si mwongo, mwenye hekima, busara na anajua kuzungumza. 
Kwa kuwa binti anajua nia yako, kabla mshenga hajaenda atamwambia mama na mama atamweleza baba ambao watafanya uchunguzi kama unavigezo (kama vile ulivyotumia) kumchukua binti yao

Hatua ya Tatu: Ushenga

Mshenga huenda nyumbani kwa wazazi wa binti na hufika asubuhi sana kisha huongea na baba. Kutegemea na ``complications`` za familia husika, mshenga atarudi kwa mara zisizopungua 4

Siku ya kwanza
Mshenga huenda kujitambulisha na kueleza ujumbe aliokuja nao, ataongea na baba wa binti wakiwa nje ya nyumba. Baba atamwambia mshenga aje siku nyingine ili aweze kujadiliana na mama

Siku ya pili
Mshenga atarudi, kama siku ya kwanza atongea na baba wakiwa nje ya nyumba na atampa majibu kutoka kwa mama, kama ni mazuri atamwambia aje siku nyingine ila wampe taarifa binti kama ataafiki au la

Siku ya tatu
Awamu hii mshenga huja kupata majibu ya mazungumzo baina ya wazazi wa binti na binti, kama awamu zilizotangulia mazungumzo ni kati ya baba na mshenga na hufanyika nje. Kama majibu ya binti ni mazuri, mshenga kama si baba ataambiwa aje na wazazi wa kijana ili wawafahamu

Siku ya nne
Awamu hii mshenga huja na wazazi wa kijana na hukaribishwa ndani, watahesabu kama kuna ujamaa na kama hakuna ujamaa, mahari hupangwa na baba wa binti kulingana na uwezo wa familia ya waoaji na jinsi huyo binti anavyopendwa kwao. Pia huandaa mpango mzima wa sherehe.
Kabla ya kufanya sherehe ya harusi, kijana hutakiwa akafanye kazi za kilimo au ujenzi nyumbani kwa binti na kama hataweza kwenda itambidi alipe ng'ombe moja dume kwenye sehemu ya mahari

Mahari
Kwa kawaida mahari (gwada) huwa ng'ombe dume moja, usunbufu wa kumsumbua baba (munu tata) ng'ombe dume moja, kama hajahudhuria kazi dume moja na kama binti amekwishaanza kuishi na kijana (harawatling) atalipa dume moja.
Pia mama hupewa kondoo dume moja, mjomba hupata beberu moja na shangazi hupewa shuka (tayti). Shangazi na mjomba ni wale tu wanaostahili (hariima)
Baada ya taratibu hizo kufanyika, ndipo taratibu za harusi hufanyika kama zilivyo kwa jamii zingine siku hizi kama send off na harusi
Kwa kifui ndo hayo tu, kwa wale ambao mlikuwa hamjui ndo mjue sasa si kukurupuka tu

1 comment:

 1. big up uliyeaandaa hii mada ya taratibu za kufuata unapotaka kumwoa Mwiraq, binafsi nilikuwa sifahamu hizo taratibu, nimeipenda sana naomba uendeleee kutujuza mambo mazuri zaidi tusiyoyajua kutoka ktk jamii yetu ya Wairaq.
  God bless u.
  Regards
  Delfina Qambesh.

  ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda