Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Wednesday, May 30, 2012

Wananchi Wenye Hasira wafunga barabara Endagew


  • Ni baada ya gari Hiace kugonga ng`ombe na mbuzi
  • Wakesha usiku kucha, wafanikiwa ``kulidaka``
  • Alipa fidia na faini Sh 500,000/=
  • Wananchi wapoteza imani na polisi
Wananchi wenye hasira wakazi wa Endagew katika kata ya Getarer kuanzia jana walifunga barabara ``kwa amani`` na kukesha barabarani wakiisubiri basi dogo aina ya Hiace lenye namba za usajili T 154 BSQ linalofanya safari zake kati ya Katesh na Haydom ambalo jana majira ya saa 7 mchana liligonga na kuua mbuzi wawili papo hapo na kumjeruhi ng`ombe moja na kisha kutokomea. 
Gari baada ya kunaswa na wananchi hao na kumweka kitimoto suka
Ohayoda ilipita katika eneo la tukio ikiwa katika shughuli zake na kubaini kuwa barabara imefungwa na kufahamishwa kuhusu tukio hilo majira ya saa 11 alfajiri. Baada ya kurejea majira ya saa 3 asubuhi ya leo ohayoda ilikuta gari hilo ``limedakwa`` na wapiga kura hao wenye hasira na kumweka kitimoto dereva wa gari hilo aliyefahamika kwa jina moja tu la ``jongo``
Akizungumza na Ohayoda, mwenyekiti wa kijiji cha Endagew ndugu Agustino Damiano Bukha alisema kuwa wananchi hao walifunga barabara kwa amani huku wakiyaruhusu magari mengine nia yao ikiwa ni kulikamata gari husika ambapo wananchi hao walikesha usiku kucha.
Mwenyekiti huyo alizidi kueleza kuwa dereva huyo amekubali kulipa fidia ya shilingi 210,000/= ikiwa ni 60,000/= thamani ya mbuzi wote wawili na 150,000/= kama fidia ya ng`ombe na jumla ya shilingi 300,000/= kama faini ya kusababisha usumbufu kwa wananchi hao.
Katika hali ambayo inazidi kuwa ya kawaida pande hizi, wananchi wanazidi kupoteza imani na jeshi la polisi na serikali kwa ujumla kwani katika mchakato wote huo hawakutoa taarifa polisi na hata Ohayoda ilipomwuliza mwenyekiti huyo kwa nini hawatoa taarifa polisi alisema;
``Tumeona ni usumbufu kwenda polisi na mchakato huu ungechukua muda mrefu na gharama kubwa``
Katika kudhihirisha kauli hiyo, dereva wa gari hilo amekubali kulipa fidia na faini hiyo aliyotozwa na wananchi hao na suala hilo kumalizika kwa amani.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda